Fursa ndani ya Babati - Manyara

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
1,191
Reaction score
1,240
Ndugu zangu poleni kwa majukum ya hapa na pale,
Naomba niende kwenye point Moja kwa moja
Ktk pita pita zangu za hapa na pale nilijikuta nikizunguka ndani ya mkoa wa Manyara,
Manyara ni moja ya mkoa uliopo Kati ya Singida na Arusha

Frusa zilizopo manyara ni km ifuatavyo
* Wilaya ya Babati mjini haina kituo chochote cha Radio

* Hakuna Usafiri wa Haice (dala dala) licha ya kwamba uhitaji upo

*Ni mji ambao hauna super market inayo onekana wala kufahamika hivyo watu wengi hufanya shopping Arusha

*Hakuna Show room ya Magari, japo wenyeji wake wanaweza kustahimili kununua magari, maana ni wakulima wazuri wa mazao ya kibiashara

*Nguo za mitumba ni Adim wilaya hii

*Mkoa huu Hauja pata wawekezaji wa Ving'amzi wengi wanajua Azam na Star times tu

* Mabinti ni wengi ila Harusi ni chache sana

Nitaendelea baadae endapo mtahitaji niendelee.
 
Umenishawishi kidogo kweny mstari wa pili kutoka mwisho
 
Yes, ina maana mtu anasubilia hadi siku ya mnada ndo anunue, Hivyo hiyo ni fursa kwa mtu anae weza kuuza nguo Kila siku
Wengi hufanya manunuzi ya nguo za mitumba kwenye minada.
 
So Unashauri wake wanaohitaji kuoa waende huko?
 
Kwani Manyara Fm haipo tena??
 
Usisahau pia UKIMWI ni mwingi kuliko wilaya yeyote katika mkoa huo!
 
92.2 haipo tena, nilifanya uchunguzi nikaambiwa imefungwa kwa takribani miezi 7 iliyo pita, Hivyo manyara Hakuna radio wala TV, so hyo ni frusa
Kwani Manyara Fm haipo tena??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…