Fursa ndani ya Babati - Manyara

Hv we sister unajielewa kweli?una uhakika radio Manyara iko hewani au na wewe upo kwenye list ya Konki master, Tatizo unajifanya unajua sana, Na ukithibitisha kwamba wako hewan, nta kuwekea barua ya tcra ya kuwasimamishia matangazo
Ndio maana mwanzo ilikuwaga Ngunguu, baada ya matatizo wamehamia Mrara juu, lakini pia bado hawajaanza kurusha matangazo, Ngoja nikuache na kingereza chako cha ugoko, mwisho ntapigwa Burn bure
 
Dingoo acha ushamba

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mapishano haya kati ya brother war boi lupa na king MfalmewaKiha yanatusaidia sisi wengine kupata elimu pana kuhusu Babati na maisha yake kwa ujumla, Wakuu labda niwaulize kama mnavyosema kuwa kutoka babati hadi Arusha ni mwendo wa masaa 2 na kitu hivi, Jee hapo Babati kuna ofisi zozote zinazotoa huduma ya kuuza tiketi za ndege na safari za watalii? aka tour agents? Sisi wengine tumejikita huko
 
Sio kweli, Manyara nguo za mitumba ni shida sana hazipatikani hasa za mabinti/wanawake ni adimu mpaka mtu asubirie siku ya mnada. Namuunga mkono mtoa mada kila ulilolitaja ni fursa kwa Mkoa wa Manyara.
 
Kiongozi Babati Hakuna ofisi hizo, hilo kama ningelisema War boy angesema kwamba Babati Hakuna uwanja wa ndege, kimsingi huyo jamaa ni mtu wa Vita tu, mimi ni mtawala. Njoo uwekeze bro
 
Asante Sana bro, maana sijui war boy anabisha nini. Frusa maana yake ni kulazimisha kisichopo ili kiwepo kiwanufaishe watu
Sio kweli, Manyara nguo za mitumba ni shida sana hazipatikani hasa za mabinti/wanawake ni adimu mpaka mtu asubirie siku ya mnada. Namuunga mkono mtoa mada kila ulilolitaja ni fursa kwa Mkoa wa Manyara.
 
Asante Sana bro, maana sijui war boy anabisha nini. Frusa maana yake ni kulazimisha kisichopo ili kiwepo kiwanufaishe watu
Ndio sasahivi Babati kuna mchanganyiko wa watu wengi, Mashirika, Makampuni na Ofisi nyingi za Serikali zimeajiri watu wengi tofauti na wazawa achilia mbali wafanyabiashara. Fursa ni nyingi kwakweli
 
Top 200 kama sikosei ni watu wanauza mitumba kwa mfumo wa Mnada,na kwa Babati nzima wanao Fanya hivyo ni km sehem 3 tu wilaya nzima,
Inakuwaga hv muuza nguo anashika nguo then watu walio kusanyika wanaanza kumsikiliza yeye tu
Kisha anasema, 500,4500.4000.3000,ukiipenda unanyosha mkono anakurushia
naomba kuelimishwa ....Top 200 ni kitu gani/nini
 
Sio kweli, Manyara nguo za mitumba ni shida sana hazipatikani hasa za mabinti/wanawake ni adimu mpaka mtu asubirie siku ya mnada. Namuunga mkono mtoa mada kila ulilolitaja ni fursa kwa Mkoa wa Manyara.
Nadhani hujaelewa vizuri comments zangu dada soma vizuri
 
Kwa hiyo baada ya muda wataanza matangazo au ndio basi tena!!..Muhimu sana kuwa na redio kwa hapa babati
 
Ningependa nikupongeza mtoa mada hasa kwa kutangaza fursa za huu mkoa..hasa hapa makao makuu ya mkoa Babati..

Mbali na fursa alizotaja mtoa mada zingine ni;
  • Chuo Kikuu-hadi sasa huku hakuna chuo kikuu hata kimoja ambacho kingeweza kuboost sekta zingine za uchumi.
  • Garage (gerej) nzuri ya kutengeneza magari..
  • Car Wash nzuri
  • Maduka ya kuuza bidhaa za jumla mfano; Stationery, vifaa vya ujenzi,n.k.
Wengine wataongeza fursa zingine...
 
Jamaa inaonyesha ni mbishi sana pia hayupo katika kujifunza ama kutaka kuelewa kitu kipya. Akili yake inawaza ubishi tu mda wote, achana nae tafadhali maana hayuko kwa ajili ya kutaka kuelewa bali kutaka sifa tu.

Mkuu samahani, nauliza vipi kuhusu fursa ya Filling Station??
Hajaelewa nini, na umetumia kigezo gani kumwita Dada!!!
 
mkuu nimekuelewa kila point ya uzi wako ni watu wachache wanapenda kushirikiana katika fursa, keep it going mkuu ila fanya mpango uifanyie kazi moja wapo
 
Manyara kwa sasa ina redio mbili kama sikosei mojawapo.

Kuna ujio wa Smile FM.
 
Wengi hufanya manunuzi ya nguo za mitumba kwenye minada.
Mkoa manyara kila karibia kila kijiji ina tarehe yale ya mnada unaozunguka mwezi mzima,kwahiyo watu wengi wanategemea mitumba toka minadani na mitumba ya minadani ni bei ya kutupa mno,kuhusu daladala sijui za kwenda wapi maana wakati mwingine daladala zinalala bila kazi pale stendi ya babati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…