Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Siku moja niliamua kufunga safari, kwenda kutalii kwenye kijiji kimoja, ili niweze kupata hewa safi ya asili itokanayo na misitu, pamoja na mimea ya asili.
Baada ya kufika kwenye kile kijiji, nikawa nashangaa shangaa mifugo inayouzwa katika mazingira yale. Wengi walikuwa ni kuku,mbuzi, kondoo, bata.
Kuangalia kwa mbele kidogo, nikaona fremu moja ya ushonaji, wapo washonaji kama saba (wanakijiji), pamoja na mzungu mmoja.
Nikaamua kuisogelea ile fremu, nikawasalimia tukawa tunabadilishana mawazo. Ile fremu ni ya mzungu, ameamua kuwapa ujira wanakijiji kwa kushona nguo; na zile nguo anazipeleka kwao Ulaya.
Baada ya kukaa, kama lisaa limoja hivi, kuna kitu nikawa nimejifunza; Fursa tunajifunza kwa kuona kwa watu.