Fursa ya biashara ndani ya visiwa vya Comoro

Wanauzia wazungu watalii kwenye mahoteli,Nipo Zanzibar hakuna kibanda Cha kitimoto holela Kama kwetu bara
 
Fursa zipo nyingi sana ila sisi watanzania ni namba moja kwa kulalamika na kutoa lawama
Taarifa lazima mtu ujue sio kukurupuka tu ndio maana wafanyabiasharawengine wageni wanaishia mikononi mwa sheria lzm upate details A to Z then ndio usonge mbele
 
Hivi hawa jamaa wanatoa first priority yeyote kwa watz hii ikiwa na maana kwamba tumewasaidia kwenye uhuru wao kwa kupeleka majeshi yetu na tukatwanga kiustadi namaanisha kunapride yeyote kwao nikijitambulisha mimi ni mTz ?

Sent from my using Tapatalk
 
Mwenye uzi kaweka bayana kuwa fursa ni nyingi na soko ni la uhakika ukitoa changamoto ndogo ndogo kama kodi,viza n.k ambazo haziwezi kumkwamisha mfanyabiashara mwenye malengo..,So Changamoto kubwa aliyoianisha hapa ni USAFIRI.., wapo Wafanyabiashara wa Tanzania wenye nia ya dhati(seriously) tuunganishe nguvu yetu kwa pamoja tuweze kodi meli na kupeleka bidhaa..,binafsi natoka Njombe nadili na uuzaji wa mbao.Nna tafuta sana soko la mbao,ambao niliona uzi mmoja humu unasema soko kule ni kubwa..,

Hivyo kama tupo tayari tujadili ni kwa namna gani tuungane na kukodi meli ya kutufikisha sokoni
 
Aise ... fursa hizi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Popote pale penye Jambo la fursa kama hili, Wapo watu Ambao hutumia fursa hiyo hiyo kuwapiga wenzao Pesa kiutapeli, Kueni Makini saanaa. Hali Ni ngumu saanaa!!
 
Kama una hela nenda kule kwa wiki moja au mbili ufanye uchunguzi wako, bidhaa zinazohitajika, wateja wako, bei, gharama za kusafirisha.

Ukirudi elimisha watu unaowaamini umoja ni nguvu.
Kweli kabisa hii ndiyo njia sahihi na muafaka ya kutaka kujua jambo lolote la biashara mahali popote! Hata kama unataka kufanya biashara ya aina yoyote tuseme huko Mbeya ni vizuri kwenda mwenyewe na ufanye utafiti wako na ujue wanahitaji nini, kwa kiasi gani,kwa ubora gani na bei zako zikoje! Tufike mahali sisi wafanya biashara au wajasiriamali tuache utegemezi na woga katika masuala haya.
 
Mkuu huyo mtu anafahamu kuongea kiswahili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…