Biashara na Comoro inachangamoto sana, hawa jamaa hawaongei kiswahili ni kifaransa,
pili hakuna usafir wakueleweka hasa usafir wa mizgo. Mahitaji yao mengi wanayapata kupitia zanzibar ambao wanatumia majahazi kupeleka vitu huko, napia wadau wanalalamika kua bahari yao inachangamoto ya mvua zenye upepo unaosababisha mawimbi makubwa na vimbunga.
Nchi yao yote nikama ufukwe hawawez kulima chochote kila ktu knahitajika kwao nigarama sana. Bei ya kilo ya nyama au nyanya inaweza kufika mara 5 yabei ya tz.
Kitamaduni hawa jamaa wanafanana sana nawazanzibar/watu watanga(washiraz) wengi ni waislam nimchanganyiko wa wabantu na waarabu ila walitawaliwa na waarabu na wafaransa. Wengi wanandugu uarabuni na ufaransa ambao ndo source kubwa yakipato kwao.
Vitu vyao vingi wanaagiza kutoka ufaransa, pakistan, china na kenya sababu usafir wakueleweka wa anga.
Vitu kma mchele mafuta nguo, mashine. Mbogomboga nyama navitu vinginevidogo dogo wanapata kutoka zanzibar
Sent using
Jamii Forums mobile app