Fursa ya Biashara/uwekezaji Katika Utengenezaji wa Pombe Kali

Kijana unapotaka kualika wawekezaji kwenye biashara au wazo lako unatakiwa kuwashawishi kwa kujieleza kama unamfundisha mtu asiyejua kitu then unaweka nambaz za investment costs. operations na outputs (profit/loss) angalau hata kidogo. Mwekezaji anataka faida muda wote na mtu mwenye pesa ana mahali pa kuipeleka muda wote (pesa ni liquid) so ili aahirishe kupeleka pesa kwingine achukue wazo lako unatakiwa kufanya kazi yako ya kutoa maelezo ya kutosha! Sio uweke heading na sifa zako binafsi halafu unawapa watu kazi ya kukuuliza maswali na hata maswali yenyewe hujibu au unajibu kitu kingine kabisa, kama vile hukuelewa swali.

Ushauri wa bure...
 
OK shukurani
 
Mkuu Lita 1 ya spirit now inaweza kufika 8000.kwahyo kusema nikutajie bei kabisa hpana ila ni kukaa chini na kuangalia kutokana na mtaji wetu tuanze na kiasi gani .pia cha mhim zaidi ni vibali mkuu
Unakwepa maswali ya msingi ya wadau mpaka unaonekana mbabaishaji,kaa chini andika mchanganuo wako vizuri,utaje initial capital
 
Mtoa mada anataka kufanana na watu wa “ukilima hapa hadi juu pale hukosi magunia 40”

Nikueleweshe mtoa mada,Muwekezaji anataka kuona faida tu atakayopata,hataki maelezo mengi.

Chakufanya,
Andaa proposal inayoonyesha input ya fedha inayohitajika,matumizi had mradi u anze ku run,then profit. (Wewe kuja na scale ya uzalishaji uifikiriayo,then investor ataamua yeye kama scale ndogo kwa mtaje wake aongeze ama scale kubwa apunguze)

Watu hawataki porojo,wanataka waone numbers.Mfano mtaji milioni 50,tunanunua vitu flan flani kiasi flani had product kukamilika ni kiasi flani,cost ni kiasi flan na faida ni kiasi flani,full stop.

Kwa maelezo yako unataka muwekezaji ndio akokotoe hivyo vyote,hell no.
 
Kwani spiriti iyo ni Ile ya vidonda au Kuna nyengine
Asili yake ni moja inakotokea ila utofauti ni kwenye matumizi kutokana na asilimia za ukali jinsi ilivyozimuliwa.
Spirit za vinywaji zina makundi yake pia kutokana na asilimia ya jinsi ilivyozimuliwa na ladha iliyoongezwa,majina hayo ni kama Vodka,Gin,whisky na kadhalika.
Kwa hiyo spirit ya kwenye pombe na ya kusafishia vidonda zina uhusiano na ndio maana kuna wale pirates ambao huwa wanakamatwaga wakitengeneza pombe feki pia huwa wanatumia spirit ya kufungia vidonda wanaizimua kisha wanapata pombe kali na kuziuza mitaani
 
Nicheki pm mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…