Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Naongea kutokana na uzoefu hiyo pesa kwa kuanzia inatosha hasa ukiamua kuchukua
Fulana
Sox
Chupi
Urembo
Chaja za simu
Saa
Cover za simu nknk
Hivi ni vitu vinavyouzwa kwa marundo na kwa kilo.. Mfano saa za mkononi saa 10 unauziwa Yuan 10 sawa na Tsh 3000.. Na huo mzigo wote unakuja nao kwenye mabegi yako yasiyozidi 20kg


Sent using Jamii Forums mobile app
Wale misukule wa TRA na ushuru wa forodha pale Airport utapona kweli hivyo vitu?
 
Wachina wapewe eneo kibaha wajengo magodown tukanunue huko mizigo kuliko kwenda China
 
Punguza ujuaji. Usidhani unachojua wewe wengine hawajui. Mimi naongelea uhalisia on the ground ulivyo na sio hizo stori za utafiti. Kijana kajibana 5m yake halafu aende kuzipoteza kwenye nauli na malazi ili tu kuiona China? Halafu akitoka China anaanza upya kutafuta mtaji. Mimi ninawasihi vijana wenye chini ya 5m waendelee kupambana mitaji ikue na huko China wataenda tu kilaini bila kujilazimisha.
Binafsi nimekupata vema sana, na kimsingi upo sahihi kabisa. Changamoto iliyopo kwenye haya marumbano ni mtazamo. Uliyekinzana nae naona anataka kuongelea swala la watu kufanya utalii wa kiuchumi au wa kibiashara jambo ambalo wewe unalipinga kwa kumuelekeza kuwa gharama unazoingia kwenda huko china ungewekeza kwenye kuzungusha kama mtaji wa biashara then in the next few years utaweza kuwa na uwezo wa kifedha kwenda huko China na kufanya kila kitu huku ukiwa na mtaji wa kutosha.

Hii concept uliyoitoa wataelewa wazoefu tu na waliokichezea ila first timers hawatapata hoja yako.

But yote kwa yote, mleta uzi Mshana Jr anafanya kitu kizuri kuwapa watu exposure ya kibiashara kusafiri na kuwafikia wazalishaji wa bidhaa za viwandani bila uwepo wa madalali. Kimsingi anawapa ujasiri wa kupata nguvu ya kupanda ndege na kwenda china, south Africa, Dubai, Uturuki, Marekani, na kwengineko kama itatokea hiyo fursa in the future.

Na pia kujifunza ni gharama muda mwingine, sasa kuna watu wapo tayari kuingia hata gharama ili kupata ile experience ambayo wengine kama mimi na wewe hatuwezi kukubali kuilipia na tunaweza ipata kwa kujifunza kwa ambao wamepitia tayari.

But big up mkuu ulichokiongea ni muhimu kwenye field ya biashara. Kulinda na kukuza mtaji.
 
Hapa nilipo ndio asubuh nipo mji mmoja hiv uko kaskazin mashariki ya china karibu na Russia ni barafu tupu. Miaka minne nyuma nilijilipua kufanya utafiti kuna tyre flan za Magar nilikuwa naifuatilia utokaji wake bongo ni mkubwa sana. Nimetoka kuweka order kama wiki mbili zilizopita kabla viwanda kufungwa. Ishu hapa ni mpunga. Ili mchina akupe tenda inakulazimu uweke mpunga wa maana Chin kama Bond. Ili wasimpe mwingine uagent in East Africa. Sasa kwasababu hela ni ndefu by then nikawatafuta wabongo tushee hiyo fursa wakatema. Nikaenda lusaka na Lubumbashi kuna washkaji tuliwah kukutana kwenye huu upambanaji mmoja msomali ana duka lusaka na mmoja mkasai nae ana duka Lubumbashi. Tulichokifanya tumefungua kampuni itakayokuwa na makao yake Dar. Ambayo Mimi ndio naisimamia na Agent mkuu zambia ni msomali na Congo ni mkasai na Mimi nawasuplaia. Imekuwa very simpo na tyre kwa mtindo huo inafaida ya kutosha. Sasa haya yote nawaeleza ili mpate kujua faida ya kutembea. We ukipata fursa ya kutoka usiangalie gharama kuna faida lukuki mbelen. Cku ukiotea viela flan unajua pa kuanzia. Ukiwa unafanya kaz na mtu usiangalie yeye anakupiga kias gan we angalia uwepo wake pale unakusogeza kias gan. Mi kwangu ukiwa mfanyakz wangu kama huna emotional za kaz nakufukuza nahtaji mtu ambae sio mwaminifu sana ila mpambanaji Sana. Kila akikaa ili aibe lazima aivushe kampuni.
Mmmmmmhmn we jamaa na hizo emotional zako za kazi. Haya tairi gani hizi unauza tuje chukua.
 
Mimi naongelea vijana ambao bado wanajitafuta. Mkuu kijana ambaye ndo 5m yake ya kwanza sio sahihi kumshawishi aitumie kwenda kujifunza/kutalii China halafu akirudi aanze upya kutafuta mtaji. Hili mimi ninalipinga. Ni sawa na kuruka steji za ukuaji.
Una hoja nzito sana. Sijui kama wanakuelewa lakini. Kuna watu huwa wanakopa kusafiri wakirudi wana madeni ya kulipa na hawana mitaji, me nakuelewa sana.
 
Waliofanikiwa kuondoka wako China tayari japo kutoka JF ni wawili tuu
Kuna mjumbe alisema hapa kwenye comments nadhani ukipekua utamkuta. Akasema hapa watakaosema wanataka kwenda na kuuliza nafasi ni wengi ila siku ya safari utakuta ni watano ndio wanakuja kufanya kweli safari. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

So nimeamini maneno yake ama kweli anawajua hawa wana JF.
 
Back
Top Bottom