Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Wale misukule wa TRA na ushuru wa forodha pale Airport utapona kweli hivyo vitu?
 
Wachina wapewe eneo kibaha wajengo magodown tukanunue huko mizigo kuliko kwenda China
 
Dunia inafunguka,mwakani nitaenda china kununua mswaki
 
Binafsi nimekupata vema sana, na kimsingi upo sahihi kabisa. Changamoto iliyopo kwenye haya marumbano ni mtazamo. Uliyekinzana nae naona anataka kuongelea swala la watu kufanya utalii wa kiuchumi au wa kibiashara jambo ambalo wewe unalipinga kwa kumuelekeza kuwa gharama unazoingia kwenda huko china ungewekeza kwenye kuzungusha kama mtaji wa biashara then in the next few years utaweza kuwa na uwezo wa kifedha kwenda huko China na kufanya kila kitu huku ukiwa na mtaji wa kutosha.

Hii concept uliyoitoa wataelewa wazoefu tu na waliokichezea ila first timers hawatapata hoja yako.

But yote kwa yote, mleta uzi Mshana Jr anafanya kitu kizuri kuwapa watu exposure ya kibiashara kusafiri na kuwafikia wazalishaji wa bidhaa za viwandani bila uwepo wa madalali. Kimsingi anawapa ujasiri wa kupata nguvu ya kupanda ndege na kwenda china, south Africa, Dubai, Uturuki, Marekani, na kwengineko kama itatokea hiyo fursa in the future.

Na pia kujifunza ni gharama muda mwingine, sasa kuna watu wapo tayari kuingia hata gharama ili kupata ile experience ambayo wengine kama mimi na wewe hatuwezi kukubali kuilipia na tunaweza ipata kwa kujifunza kwa ambao wamepitia tayari.

But big up mkuu ulichokiongea ni muhimu kwenye field ya biashara. Kulinda na kukuza mtaji.
 
Mmmmmmhmn we jamaa na hizo emotional zako za kazi. Haya tairi gani hizi unauza tuje chukua.
 
Mimi naongelea vijana ambao bado wanajitafuta. Mkuu kijana ambaye ndo 5m yake ya kwanza sio sahihi kumshawishi aitumie kwenda kujifunza/kutalii China halafu akirudi aanze upya kutafuta mtaji. Hili mimi ninalipinga. Ni sawa na kuruka steji za ukuaji.
Una hoja nzito sana. Sijui kama wanakuelewa lakini. Kuna watu huwa wanakopa kusafiri wakirudi wana madeni ya kulipa na hawana mitaji, me nakuelewa sana.
 
Waliofanikiwa kuondoka wako China tayari japo kutoka JF ni wawili tuu
Kuna mjumbe alisema hapa kwenye comments nadhani ukipekua utamkuta. Akasema hapa watakaosema wanataka kwenda na kuuliza nafasi ni wengi ila siku ya safari utakuta ni watano ndio wanakuja kufanya kweli safari. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

So nimeamini maneno yake ama kweli anawajua hawa wana JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…