Fursa za biashara zipo, vijana wa Dar es Salaam ni wazembe tu

Mimi nilipoanza kulima ndipo niliona Dar kuna vijana wazembe sana yaani wamekaa na wanawaza kuuza viatu na nguo tu hakuna mawazo mbadala yaani hawawazi mambo makubwa.

Nimetoka Dar na nimefanikiwa katika kilimo ila Dar wanawaza tu kufungua maduka ya nguo, viatu na simu. Mfano kijana hapo Dar kuna magunia mengi ya mkaa yanaingia kila siku kutoka maeneo mbalimbali ukichukua magunia yako 10 na Canter upeleke Morogoro au Tanga ndani ya siku 3 mkaa umeisha unarudi Dar kufunga mzigo mwingine.

Basi achana na hilo la mkaa, chukua zako asali lita kuanzia 100 weka kwenye vibebeo safi na nembo yako pia, ingia Tabora au Singida uza ndani ya muda mfupi unarudi kufunga mzigo mwingine hiyo kumbuka ni chini ya wiki moja unaweza kuuza lita 100 za asali.

Chukua mafuta ya Alizeti kiasi cha kutosha ingia Mwanza piga biashara usisubiri serikalini ikuambie fursa, fursa ni nyingi sana hapo Dar ila wengi wamekariri fursa aina moja tu.

Kama kuna yeyote atakuwa tayari nitamsaidia alete biashara yake huku nitamsaidia kutafuta masoko. Pia mjaribu kwenye kilimo sio biashara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeaongea ujinga saana yaani mtu achukue mkaa toka dar aurudishe Tanga wanakochoma mkaa..? 😁😁😁
 
Mawazo mazuri, ila I got this gut feeling ya "easier said than done"

Kwenye biashara kuna kitu kinaitwa "network" na inachukuaga muda mrefu kujenga. Watu wote unaoona wanatoka ndani na nje ya Dar walianza kujenga network miaka 3 plus kwenda nyuma.

Kuna mtu alisema humu "no sales, no business". Kama kuna kitu vijana wafunzwe basi ni process ya sales and marketing.

Na pia kufahamu dynamics za demand and supply.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa katoroka mirembe nini!
Yani tununue ndizi Dar tukauze Kilimanjaro kweli?
 
Unajua Faida ya simu bei gani? Kilimo Kina pesa na lazima uweke pesa na nguvu.. Kibali cha kusafirishia mkaa unajua ni bei gani? Nakwanini upeleke mkaa moro nasio Dar.
 
Back
Top Bottom