SoC02 Fursa za Sayansi na Teknolojia kwa vijana karne ya 21

SoC02 Fursa za Sayansi na Teknolojia kwa vijana karne ya 21

Stories of Change - 2022 Competition

Matty Daizan

New Member
Joined
Nov 10, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Tuanzie mbali kidogo katika karne za nyuma hususani kuanzia karne ya 18 hadi ya 19 dunia iliingia katika machafuko ya kivita na biashara za utumwa.

Ndani ya karne hizo pia kulitokea na mapinduzi ya viwanda yaani mashine zilianza kufanya kazi na kuibuka kwa uzalishaji mkubwa wa bidhaa na hivyo kukua kwa nchi nyingi sana za ughaibuni.

Afrika bara letu kiukweli hapa tulikuwa nyuma sana hasa kwenye suala nzima la mapinduzi ya viwanda mana tulisha dakwa na biashara ya utumwa na hivyo kupelekea watu wetu wengine nchi za ughaibuni.

Yapo mengi yaliendelea lakini asimia 90 yamebaki kuwa historia tu,ebu tuachane nayo.
Karne ya 21 ndo kwanza bado ipo mwanzoni mana kwa sasa tupo mwaka wa 22 toka ilipo anza,lakini karne hii dunia imejikita kwenye suala nzima la sayansi na teknolojia,Je sisi kama watanzania tunaenda sambamba na kauli mbiu ya karne ya 21 au bado tupo nyuma!?

Kiuwazi usio pingika siku hizi kuna fursa nyingi sana kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia huwenda kama tungeichukulia maanani hata suala la ajira ilisingekuwa kubwa kama ilivyo mjadala hivi sasa.

Moja ya uwepo wa sayansi na teknolojia ni kutatua changamoto ambazo uwenda katika jamii husika zinaisumbua jamii Mfano,uwepo wa JAMIIFORUM umetufanya leo tukutane pamoja kuweza kujadili mengi kwa uhuru na amani,na haya ndio matumizi yenyewe ya teknolojia.

Fursa ndani ya teknolojia ni nyingi ila mimi tagusia mbili tu;
1.Usanifu wa programu na wovuti
Tunajionea sasa hivi sehemu kubwa ya shughuli zetu nyingi tunazimalizia programu au wovuti ambazo asilimia kubwa zimetengenezwa na watu kutoka ughaibuni nazani hii ni fursa kwa Watanzania kuja na usanifu wa programu au wovuti kutokana na suluhisho kwatanzania ili kukizi uhitaji wa jamii yetu.

2.Elimu juu ya teknolojia mpya
Hapa kuna mengi sana ila tagusia machache ikiwemo masuala mazima ya Mapinduzi ya nne ya kompyuta hapa tunaizungumzia BLOCKCHAIN ambayo imeleta usalama wa hali ya juu mtandaoni na kuleta sarafu nyingi za kidigitali kama BITCOIN ambazo wengi tunatalajia ndio suluhisho kubwa la malipo ya mtandaoni katika jamii zetu hapo mbeleni(miaka michache kuanzia sasa).

Hivyo basi jamii kama jamii inahitaji kujua mengi kuhusu hii blockchain na jinsi watakavyoweza kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na shughuli zao kupitia hizi teknolojia mpya.

Yangu ni hayo tu kiufupi.
UJUMBE:Kuna mengi katika tenolojia na sayansi katika huu ulimwengu hakikisha unajitahidi kujifunza angalau machache kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.
WAGMI
 
Upvote 0
Back
Top Bottom