Fursa za Uwekezaji Tanzania-Mkoa wa Tabora

Fursa za Uwekezaji Tanzania-Mkoa wa Tabora

Nenda wilaya ya Kaliua, kodisha heka 50...

Nenda Kigoma, chukua wafanyakazi 10...

Lima heka 30 tumbaku...

Lima heka 20 mahindi na karanga(changanya)

Mwombe Mungu ashushe mvua ya kutosha...

Baada ya mwaka huo, njoo ututukane jobless hapa Jf...

Kila lakheri.
 
1. Fungua duka kubwa la dawa (Big Pharmacy). Maana hakuna hilo duka,
Pale Tabora mjini, yaliyopo ni maduka madogo madogo
Acha uongo. Kuna Mchele Pharmacy ametawala Tabora mjini.

2. Fungua kliniki kubwa ya kisasa ya kibingwa (Polyclinic).
Acha uongo. Kuna Polyclinic ya Mission ipo pale Ipuli huwaambii kitu wana-Tabora

4. Fungua printing company matata, unakula tender zote za kuchapisha vitu mbalimbali.
Acha uongo. Rogers Photo Studio yuko pale opposite na NMB utampeleka wapi?
 
Fungua duka kubwa la dawa (Big Pharmacy). Maana hakuna hilo duka,
Pale Tabora mjini, yaliyopo ni maduka madogo madogo na wagonjwa wengi wanatumwa kwenda Mwanza, Dodoma, Dar au Kilimanjaro sometimes kufuata kununua dawa tu.
Wewe utakuwa umesimuliwa kuhusu Tabora au huna akili...

Yaani mtu atoke tabora aende Kilimanjaro au Dodoma kufata pharmacy?

Uli ihugane sana, ivya lyako...
 
Nenda Tabora mjini fanya utafiti ni wilaya gani wanalima kwa wingi zao la karanga. Ukipata jibu nenda hiyo wilaya ndani ndani huko chukua heka kumi lima hilo zao, karanga kule zinakubali sana.
Urambo, kaliua zinakubali na pamepakana na kahama, kigoma yote iyo, warundi wanahamia mdogo mdogo.....
 
Wewe utakuwa umesimuliwa kuhusu Tabora au huna akili...

Yaani mtu atoke tabora aende Kilimanjaro au Dodoma kufata pharmacy?

Uli ihugane sana, ivya lyako...
Mwalala mpola, niliwahi pata mwanamke wa kinyamwezi akawa ananifundisha kilugha, nikasahau kichagga ghafla😆 anatokea urambo mpigwa, 😅😅😅😅
 
Mkoa wa Tabora ambao nimefanya Kazi Miaka 5 kuna Fursa za Usindikaji Mazao ya Kilimo hasa Mpunga,Karanga na Asali.Haya Mengine ya Kulima na uchuuzi yako na risk za Kutosha.Pharmacy zipo za Kutosha Kwa sasa.Polyclinic nyingi zimejifia Kifo cha Mende,sababu zinajulikana.Ukiwa na Mtaji Ingia Igunga na Nzega kuanzisha Uchimbaji na uchenjuaji wa Dhahabu.Mkoa Una watu wengi lakini wamesambaa maporini na per capita income Yao IPO Chini.
 
Kwa sasa upo mkoa gan
Mkoa wa Tabora ambao nimefanya Kazi Miaka 5 kuna Fursa za Usindikaji Mazao ya Kilimo hasa Mpunga,Karanga na Asali.Haya Mengine ya Kulima na uchuuzi yako na risk za Kutosha.Pharmacy zipo za Kutosha Kwa sasa.Polyclinic nyingi zimejifia Kifo cha Mende,sababu zinajulikana.Ukiwa na Mtaji Ingia Igunga na Nzega kuanzisha Uchimbaji na uchenjuaji wa Dhahabu.Mkoa Una watu wengi lakini wamesambaa maporini na per capita income Yao IPO Ch
 
Back
Top Bottom