Kitumba_
Member
- Aug 21, 2018
- 30
- 21
Tanzania ni moja ya mataifa ya kiafrika yenye idadi kubwa ya vijana. Inakadiriwa ya kwamba zaidi ya theluthi moja ya watanzania wote ni vijana, Yaani kwenye kila watu watatu mmoja ni kijana. Hii inaweza kuwa moja ya fursa kubwa kwa taifa au Bomu moja litakalolipua uchumi wetu, itategemea na hatua gani taifa litachukua dhidi ya.
Taifa litazitilia mkazo sera nzuri na kuwekeza katika fursa adhimu ya uwepo wa nguvu kazi kubwa? Litaimarisha elimu ya upili, utatu, ufundi stadi na maendeleo ya ujuzi? Litaimarisha kilimo ambacho ni tegemeo kubwa, utunzaji chakula na huduma za matibabu? Litazalisha ajira na kuusukuma ujasiriamali? Litatengeneza mazingira ya amani na umoja pasi upendeleo?.
Ili Tanzania iunganike kuwa kitu kimoja, bila ya kutengana, hii fursa ya kihistoria itategemea sana serikali kama iko radhi kuungana na kizazi hiki kipya.
"Vijana wanahitajj kuhusishwa ili kufikia maendeleo ya kweli!". -Julius Kambarage Nyerere 1974. (Chanzo: bbcswahili.com).
Maamuzi yoyote kuanzia ngazi ya familia na mtu mmoja mmoja ni lazima yafikilie mbali kuhusu vijana na kizazi kijacho. Ni wazi maamuzi hayo yataathiri mazingira (Tabia nchi), uchumi na mawazo ya jamii ambapo yatatoa matokeo kwa vijana. Vijana ikibidi wachukue nyadhifa ili kufanya mabadiliko.
Upungufu wa ajira umekaririwa kuongezeka mara dufu zaidi ya mahitaji ya mitaji kwa vijana kwa siku hizi za usoni pengine kutokana na huu mlipuko wa UVIKO19. Inatia moyo kwamba vijana wa kitanzania wanaendelea kupambania kombe kupitia ujasiriamali wao ili kujizatiti.
Ndio maana ninayo furaha kuwa balozi wa vijana, uwakilishi ambao unanipa fursa ya kujifunza mengi na kubadilishana mawazo na idadi kubwa ya vijana nchini. Kitumba na- 'share' ushauri kwa vijana kuhusu kunyumbulika na ushirikishwaji kiuchumi vijana, mazingira, miundombinu bora, ubaguzi kijinsia na ukosefu wa ajira.
" Vijana wanapelekea mabadiliko. Una kipaji, nguvu na mawazo ya kuzuia migogoro, haki za binadamu, kulinda amani na kufanyia kazi ajenda ya maendeleo endelevu 2030". - General Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Uwezo wa wasichana wa kitanzania bado haujafikiwa kivile kutokana na matendo kadhaa ya kibaguzi. Nikiwa nimefanya kazi na jamii ya chini kabisa, nimeshuhudia vijana wakiwekwa nyuma kwenye mambo muhimu, wengine wakilazimishwa kuacha shule ili waolewe, wengi sana wakikeketwa.
Ni furaha kuwa kuona idadi kubwa ya vijana wa Tanzania wanapata elimu na kuelimika.

Upvote
0