Habari wakuu.
JE WEWE NI MGENI KATIKA TASNIA YA USAFIRISHAJI NA UNGEPENDA KUSHAURIWA GARI ZA KUANZA NAZO BIASHARA YA USAFIRISHAJI?
NB:
Ushauri huu nitautoa kwa mujibu wa uzoefu wwngu katika tasnia hii lakini pia nikiwalenga wale wageni kabisaaa hasa ambao mitaji sio mikubwa.
Ipo hivi, hapa nchini kuna brands nyingi sana za magari makubwa kuanzia zile zinazotoka America, Ulaya, Mashariki ya mbali hadi Korea. Kwa marneo yote hayo kila mmoja anakua anazalisha gari ambayo amelenga mazingira fulani ya ufanyaji kazi na ndio maana ukichukua Howo ya China na Scania ya Sweden yanatofautiana kabisaaa kimuundo, kimakenekia na kiuendeshaji kwa sababu kila muundaji amelenga mazingira yake.
Sasa kwa wale wazee wenzangu wa used ni vizuri kulenga gari ambayo itakua na sifa za
🔥 KUDUMU,
🔥KUTENGENEZEKA KIURAHISI,
🔥UPATIKANAJI WA VIPURI KWA BEI RAHISI
🔥INAYOMUDU MAZINGIRA YA KWETU.
🔥BEI RAFIKI
Kwa vigezo hivyo hapo juu basi naomba nikushauri kuwa gari unayopaswa kuanza nayo ni SCANIA 124L-420 au 124L-380 ambazo sio RED DOT hizi ndizo gari ambazo kwa uzoefu wangu zinakidhi vigezo tajwa hapo juu. Na kama ukikosa kabisa basi angalau upate 114L-380.
Hizo ndio horse zangu bora kabisa za kijasiliamali.
Nitakuja siku nyingine na trailers