Futari ipi uipendayo

Asante sana Somo yangu...manake mwari napenda kunukia hatari...

Huwa natumia udi wa kuchoma, natumia na kitezo cha umeme...jana si ndo ukakatika siku nzima....nilinunajeeeee!
Bora nitumie al udi...

Kuna vya mkaa ila viko vya nakshi fulani vizuri sana tu natumia vyote ila cha mkaa ndio kinakua poa sana yaani udi unanukia vizur kuluko cha umeme.
 
Asante sana Somo yangu...manake mwari napenda kunukia hatari...

Huwa natumia udi wa kuchoma, natumia na kitezo cha umeme...jana si ndo ukakatika siku nzima....nilinunajeeeee!
Bora nitumie al udi...

Mwari naona ushapasi lol
 
Out of topic, jamani natafuta Al udi nzuri...anayejua anitajie jina na bei ikiwezekana...

cc; farkhina Mrs Kharusy Honey Faith FaizaFoxy na wengineo.

Al Oud nzuri Tanzania huipati, sijapatapo kununua Tanzania. Al oud nzuri uiagize Saudi Arabia au Oman. UAE vilevile lakini huko wahindi wanabambikia.

Hapa au Unguja utapata lakini ni the lowest quality.
 
Leo vipopoo, choroko za nazi, tambi za kukaanga, chapati kwa mchuzi wa king fish vipo?

Hahahaha atavimaliza vyote lakini saumu ukiwa kali waishia kunywa mimaji tu hata huwezi kula
 
Leo vipopoo, choroko za nazi, tambi za kukaanga, chapati kwa mchuzi wa king fish vipo?

Hapana leo chapati za maji,samaki wa kukaanga,mchemsho wa kuku na ndizi,tambi na ndizi mzuzu zilokolea nazi na custard....nlualike nini?
 
Reactions: BAK
Al Oud nzuri Tanzania huipati, sijapatapo kununua Tanzania. Al oud nzuri uiagize Saudi Arabia au Oman. UAE vilevile lakini huko wahindi wanabambikia.

Hapa au Unguja utapata lakini ni the lowest quality.

Yeah ni kweli kabisa hizo za wahindi sio nzuri kabisa na udi zao sijui zinanukiaje ila kuna ambazo ni nzuri afadhali znz unapata.....

Kim nana kama upo serious unataka kuagizia dubai ni pm ntakuagizia ila ni expensive......
 
Kim nana hizo nlokwambia ni affordable kabisa ila unatakiwa uwe na udi mzuri sana alafu unachanganya na nyengine alafu unahifadhi kwenywe chupa ya kigae.....

Kuna haliudi zile ndogooo kama unazo ambayo unaona harufu yake kali sana huwezi pakaa unachukua pamba kiasi unaroesha na haliudi alafu wakati unafukiza udi unaiweka na hiyo kwenye chetezo utapendaa...
 
Last edited by a moderator:
lol!!!!! hahahaha weye unauliza majibu? Uliza maswali banaaa πŸ™‚πŸ™‚

Hapana leo chapati za maji,samaki wa kukaanga,mchemsho wa kuku na ndizi,tambi na ndizi mzuzu zilokolea nazi na custard....nlualike nini?
 
lol!!!!! hahahaha weye unauliza majibu? Uliza maswali banaaa πŸ™‚πŸ™‚

Hahahahahha sawa karibu sana uje na mabakuli ukimaliza ufunge vya vyengine
 
Reactions: BAK

Asante somo yangu...hadi raha kuwa na somo kama wewe...
Mbona nikiolewa siachiki mie....!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…