Hakuwa Askari huyo, Askari aliyeiva akiambiwa kamkamate flani Ni mdhambi. Bila swali Ni kujibu ndio mkuu na kuelekea eneo la tukio.
Nb. Mzee Mohamedi Aziz alikudanganya kukidhi maslahi yako ya kidini coz we Ni mwandishi mdini isivyo kawaida. Kukataa amri ya kijeshi Ni kosa lisilosameheka. Labda Kama utaniambia Hamza baada ya Jambo Hilo alijiuzulu ama kuondolewa kule juu.
Bahati nzuri kwa nchi Kama hii Ni Jambo la kushukuru Kwamba watu Kama wewe hamtapewa Madaraka makubwa coz mtaendekeza udini bila kificho.
Lakini pia Kama Ni kweli, kutoa kwake siri hiyo tena kwa raia asiye na uzoefu wowote na taaluma ya polisi Ni kosa kimaadili dhidi JMT.
Sela...
Sikulaumu kwa maneno yako wala sikulaumu kwa kuniita mimi mdini.
Sikulaumu kwa kuwa huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.
Hisstoria uliyosomeshwa watayarishaji wake walifuta historia ya kweli wakapachika historia siyo.
Katika historia siyo hakuna mchango wa Waislam wa Tanganyika katika kuunda kwanza African Association mwaka wa 1929 kwa kuwa ulifutwa kwa hofu wala hukusoma mchango wa Waislam katika TAA kuanzia 1948 hadi kuundwa kwa TANU 1954.
Hii iliyofutwa ni historia ya wazee wangu.
Mimi naijua vyema.
Nilipogundua kuwa historia ya TANU imebadilishwa kwa kuhofu historia ya Uislam na Waislam ndani ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika ndiyo nikanyanyanyua kalamu kuiandika.
Kitabu nikakipa jina, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' (1998).
Mimi kwa kufanya hivi umeniita mdini.
Kitabu hiki ndicho kilichobadili historia nzima si ya Nyerere tu bali historia nzima ya uhuru wa Tanganyika.
Inanishangaza kuwa wale waliofuta historia ya wazee wangu na jamii yangu umewaona wako sawa ila mimi niliyeandika historia ya kweli ni mdini kwa sababu nimetaja historia na mchango wa Waislam na Uislam.
Vipi kuhusu wale waliofuta historia ya kweli?
Hawakusukumwa na hisia za dini yao kufuta historia ya jamii yenye imani tofauti na yao?
Humjui Hamza Aziz na uhusiano wake na Nyerere.
Wala hujui nini kilitokea baada ya uhuru kupatikana.
Labda umesikia kijuujuu tu uhusiano wa Dossa Aziz kaka yake Hamza na Julius Nyerere.
Sikulaumu kwa kukosa kujua haya kwani yote yalifutwa.
Ungejuaje?
Yawezekana kabisa wala humjui Abdul Sykes na mdogo wake Ally na Abbas na pengine hata hujui kuwa baba yao Kleist Sykes ndiye muasisi wa AA na kaacha mswada wa kitabu.
Mswada uko Maktaba ya Chuo Kikuu na ni kutoka Idara ya Historia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam toka mwaka wa 1968.
Historia uliyosomeshwa ni kuwa historia ya TANU inaanza na Julius Nyerere.
Uliamini historia hii kwani hukupata kusomeshwa kuwa historia ya TANU kuundwa kwake haiwezekani kuandikwa bila kumtaja Hamza Mwapachu na Abdul Sykes kwani huyo Nyerere kapokewa na Abdul na Ally Sykes na kuna mengi yalipitika hadi Nyerere kupewa nafasi ya juu ya uongozi katika TAA 1953.
Hamza Aziz wakati huo yupo na kaona yote.
Sheikh Hassan Mufti wa Tanganyika aliunga mkono uteuzi wa Nyerere katika TAA.
Uhuru ulikuja na changamoto nyingi na mojawapo ni hii njama ya kuwafuta katika historia ya TANU wazalendo mfano wa Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz, Sheikh Hassan bin Ameir na nakutajia hawa kwa kuwa nimekutajia lakini wako wazalendo wengi kutoka majimboni.
Hamza Aziz alikuwa anajua kuwa mimi naandika historia ya TANU historia ambayo yeye na kaka yake Dossa na wazalendo wengine ni sehemu yake.
Hili ndilo lililomfanya Hamza Aziz aniondolee pazia na kunieleza mengi.
Haya ndiyo yaliyomfanya Ally Sykes anikabidhi hazina ya nyaraka alizokuwanazo kuhusu AA, TAA na TANU na kunihadithia historia ya Julius Nyerere na uhusiano uliokuwapo baina ya Nyerere na Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na wazalendo wengine wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Sikuishia hapo nilisafari kwingi Tanganyika kuwatafuta wapigania uhuru na nikazungumzanao.
Nilipomaliza nikaandika kitabu.
Leo nakusomesheni upya historia ya TANU na historia ya Nyerere.
Hakuna somo la dini katika historia hii ila utaona mchango mkubwa wa Waislam kama ulivyokuwa.
Kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Ameir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) kuzuia Waislam wasijenge Chuo Kikuu haikuwa siri.
Wala Hamza Aziz hakunidanganya kwani yote yakifahamika.
Uliodanganywa ni wewe ambae hukupata kuyajua haya niliyoeleza hapa.
Nakusomesha upya historia ya uzalendo na nimekuwekea historia na picha za wazalendo waliokuwa bega kwa bega na Nyerere.
Kulia ni Zuberi, Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia wakiwa kwenye tawi la TANU lililofunguliwa na Ali Msham nyumbani kwake mwaka wa 1954 na Ali Msham ni huyo wa pili kulia waliosimama.
Hao wengine ni vijana wa Bantu Group wahamasishaji umma na walinzi wa viongozi wa TANU.
Kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na wa kwanza kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee wako na Nyerere wakimsindikiza Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Nyerere UNO February 1955.