Naona sijaeleweka na baadhi ya watu wamechukulia post yangu negatively kiasi kwamba nimejikuta nashangaa sana tena sana na wengine kama wewe wametaka kujua kuhusu nilichoandika,nitaeleza sababu za mimi kuandika post kama ile ili wale ambao wanahitaji kujifunza wajifunze....
Kwanza kabisa ni kwamba nilitaka kuonesha kuwa mtoa mada hakuwa sawa kwa kusema kuwa Skull and Bones ndiyo wanaoiendesha dunia,pili nikaonesha njia kwa kutaja jina ambalo kabla ya mtu kunirushia shutuma alipaswa akafanye utafiti ajue ni jina la nani nililolitaja lakini kama kawaida yetu Wabongo tumerusha shutuma na matusi....
Kimsingi,kama nilivyofanya mimi ninapenda sana watu wasipende kuambiwa kila kitu bali wakafanye utafiti wao wenyewe wajue maana ukiambiwa sana uwezekano wa kudanganywa ni mkubwa sana,sasa hapa naona mnataka niseme mimi kile ninacho kijua,siyo jambo baya sana lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba hamjui ninachotaka kusema ni kitu gani.Ukweli ni kwamba ni ngumu sana kuelezea nijuacho kwenye post moja au thread nzima hapa JF kwasababu kuu mbili...
1;Wabongo ni wavivu sana wa kusoma makala ndefu hivyo nikipoteza muda kuandika hapa haitakuwa na maana yoyote ile...
2;Mambo ambayo ninapaswa kuyaandika ni mengi sana kiasi kwamba yatakula muda wangu hadi wa kutafuta mkate wa kila siku hivyo kunisababishia nishindwe hata kununua bando la kuingia hapa JF na kuandika haya,sasa hii ni shida kubwa sana....
Ninachowashauri watu ni kwamba wajitahidi sana kujifunza wenyewe kwa muda ambao wanakuwa free,siku hizi ni rahisi maana tunatoa na key word kabisa hivyo unapata pa kuanzia,nilitaja jina Pindar,huyu ni mkuu wa Illuminati asiyeonekana na hata wanachama wa Illuminati wenyewe hawamjui na inasadikiwa mkuu wa chama hiki cha siri anatoka kwenye familia zile mbili kubwa zinazounda Illuminati ambazo ni Rothchild na Rockerfeller lakini hiyo ni speculation tu,ukifuartilia utajua mengi kumhusu na utakapomfuatilioa huyo atakuongoza kuelekea kwingine ambako ni kupana zaidi ya hapo....
Kwa mimi ambaye nina miaka mingi kigogo ninafuatilia mambo haya nikikutana na mtu anayejadili Illuminati,Freemason au Skull and Bones kama wanaoiendesha dunia namuona kama bado hajajua ukweli kabisa maana hivyo vyama vya siri ndivyo ambavyo watu wanakutana navyo mwanzoni tu wanapofuatilia mambo haya na ndivyo vinavyojulikana mitaani sasa.Wakati mimi naanza kuwafuatilia hawa watu Illuminati na Freemason haikuwa ikijulikana kwa watu kabisa na kuna watu walikuwa wananiona ni kichaa,Skull and Bones ndiyo kabisaa hawakuwa wakijulikana,sasa kitu ambacho nilikifuatilia miaka karibia 15 huko nakuja kuona mtu leo anaona ndiyo cha ajabu nashangaa kidogo...
Kuna vyama vya siri ambavyo havijulikani na wengi,vyama kama Theosophical society,Luci's trust [Lucifer's trust],Rosicrusian [Rose and cross],Club of Rome na vingine vingi ni miongoni mwa vyama vya siri ambavyo viliundwa kwa umakini ili yoyote anayefuatilia ajikute anaamini kuwa hao ndiyo kila kitu na aishie hapo kama mtoa mada wakati kuna mengi zaidi...
Bahati mbaya ukiishia hapo hutawajua watu kama Aliester Crowell,John Dee na kiboko yao Mainly P. Hall na bila kumsahau Hellena Petrova Blavasky au mwanafunzi wake waliyeshirikiana naye kuunda Luci's Trust,Alice Baily.Hellena Blavasky anamahusiano ya kindugu na mke wa Prescot Bush babu wa George W. Bush ambaye ni mtoto wa George H Bush ambaye ni mtoto wa Prescot Bush...
Unapoanza kujadili masuala ya vyama vya siri unakuwa bado kabisa na nakuona kama upo shule ya msingi ya kuelekea kuwajua wanaoiendesha dunia kwasababu huko baado sana ni mbali.Ukifikia kuwajua Nephilims na bara la Atlantis ambalo halipo leo na walipotoka sasa hapo utakuwa upo secondary ukielekea kuwajua akina akina Sananda ni akina nani au Sanat Kumara hapo sasa unakuwa umefika secondary A-Level ukielekea chuo ambako utakutana na wanaoiendesha dunia....
Jitahidini kufuatilia majina niliyoandika ili muweze kujua mengi na siyo kutaka kuambiwa kila kitu.Hapa tu nimewapa hints na mnaona maandiko yamekuwa mengi.Kutaka kuwaelezea tu akina Mainly P. Hall si itakuwa shida?
Niwatake radhi kwa niliowakwaza lakini wito wangu ni kwamba tujitahidi sana kujifunza na kuacha kutukana watu bila sababu za msingi....