Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 14,241
- 40,752
Aliyekuwa Makamu wa Rais nchini Kenya Mheshimiwa Rigathi Gachagua amesema maisha yake yapo hatarini akimtuhumu Rais William Ruto kuhusika na tishio hilo.
Gachagua amesema alipewa taarifa kuwa maafisa wa serikali wakishirikiana na polisi walipewa amri ya kumuwekea sumu kwa njia hewa akiwa kanisani. Amesema sumu hiyo ingeathiri ubongo wake ndani ya miezi mitatu na kupelekea kifo chake.
Pia Gachagua amesema kuwa ana taarifa za kiintelijensia kuwa Rais William Ruto ametoa amri ya kumpunguzia walinzi binafsi na kuwaondolea kibali cha umiliki wa silaha ili iwe rahisi kumshambulia na kuchukua uhai wake.
View: https://m.youtube.com/watch?v=NnKl3Tq7jRc