Mbona huyu jamaa anaonekana mwoga? Nilidhani yuko bold kumbe anatukana halafu anajificha! Aendelee kutetea misimamo yake asikimbie.
Maoni yangu, ni kwamba ndoa ni mahusiano rasmi ya watu wawili.
Kila mtu ana mazuri na matatizo yake ya ndani na nje. Kikubwa ni kuheshimiana tu kwa sababu kuachana ni sauti tosha kwamba hamwezi kuendelea kuwa pamoja.
Tabia za kuanza kupigana madongo ni ushamba na umaskini wa fikra. Kila mtu aendelee na maisha yake kwa kuwa hakuna mtu ataishi maisha ya jana. Jana yao ilikuwa mbovu ndiyo maana wakaafikiana kuunda kesho zao katika mfumo mpya.
Matusi na kashfa baada ay kutengana ni dalili ya kukosa mwelekeo mpya, kukaa njia panda lakini bila uwezo wa kurudi nyuma. Watapata mwelekeo sahihi wa maisha kwa kutulia na kupanga ustaarabu mpya ili kutorudia makosa, kutokuendeleza uchungu miongoni mwao na kuwa na future nzuri zaidi. Hakuna amani katika matusi, hakuna hatima katika kukurupuka, na hakuna satisfaction katika maisha artificial!.
Waachae ujinga, wasonge mbele kila mtu na maisha yake. Watajisifia kuwa walifanya maamuzi sahihi kama watakuwa na mwisho uliobora kuliko walikotoka, kitu ambacho hawakipati kwa kudhalilishana!.