Gadner Kung'atuka Clouds FM

Gadner Kung'atuka Clouds FM

Huyu jamaa na wengine si walijiunga clouds ili wapate jina tu!
Naona kashapata ameamua kutafuta maisha sasa.
 
hivi huyo ni nani??mi maana sisikilizagi hii redi ya mipasho
 
kila la kheri captain...:A S crown-1:
 
ni bora tu kaacha maana alikuwa anamtangazia mke wake soko tu, na kicheko chake alikuwa ananiboa usipime.
Na huyo kibonde nao aache tu maana anaongea asivyotakiwa kuongea kwenye media kabisaaaa, ajifunze kuwa mstaarabu.
 
Imefikia wakati sasa kwa clouds kuajiri watu wenye angalau uelewa na taaluma ya uandishi wa habari. Ukiwaangalia hao watangazaji kwa kiasi kikubwa ni Deiwaka ambao wamepewa kituo wakiendeshe huku wakiwa wanasimamiwa na wamiliki ama wanahisa. Kikubwa sitaki kuiponda redio hii inayojiita ya watu, Isipokuwa sasa imefikia wakati iendeshwe na kusimamiwa kitaalam sio na wahuni wachache ama watoto wa wakubwa a.k.a vigogo.
 
mbona wengi weshaachaga pale na sasa wanafanya poa tu? ray c, tid ...
 
"Nenda mwalimu unaturushia stimu kila msimu...." by Juma Nature
 
Nafikiri Gardner amekuwa sasa na nafasi yake kiumri na kijamii inahitaji kufikiriwa upya. Kama anatambua hilo nadhani ni wakati muafaka kabisa kuachana na media zenye mambo ya kitoto. Mifano ni mingi ya wanaofikiri, Muone Brother Masoud Kipanya na Sister Fina, walipotoka Clouds watu walifiri wamepotea kumbe maamuzi ya akina Ruge na Jose ni ya kiukandamizaji zaidi na hawatoi nafasi ya mawazo ya wengineo kuchukua mkondo. Hongeara gardner, Karibu kwenye kundi la great thinkers. Epukana na utoto uwe role model
 
hivi huyo ni nani??mi maana sisikilizagi hii redi ya mipasho
Mh nawe KB acha utani, kama husikilizagi umejuaje ni ya mipasho? ni kampuni ya magangstar wa bongo, kazi yao kuteka nyara soko la entertainment kwa kutumia Radio na TV. Gardner alikuwa mtangazaji upande wa radio na ni mme wa mwanamuziki aitwae Lady JD. Nahisi hapo nitakuwa nimekukumbusha, unganisha na melezo ya wengine
 
Sioni tatizo ameshafanya kazi za watu vya kutosha na amepata uzoefu na umri umeenda anatakiwa kufanya shughuli zake ikiwezekana kuanzisha radio station ya kwake, NITASHANGAA KAMA ATARUDI TENA!
 
Back
Top Bottom