Igor Sirkosky, The Man with the Impossible Dream of Helicopter.
Basi mwaka 1889 may 25 mjini Kiev, Ukraine, alizaliwa Igor Ivanovich Sikorsky. Akiwa kijana mwamba huyu ikichangiwa na mama yake ambaye alikua ni medical school graduate kipichi hicho pamoja na baba yake ambaye ni daktari na Professor katika maswala ya saikolojia, alipendelea kusoma ishu za science na hasa mambo ya usafiri wa anga yani
Aviation.
Alipokua na miaka 14, katika mji wa Carolina (North) alikuatana na Wilbur na Orville Wright ambao walikua wakijaribu kutengeneza vifaa vya urukaji. Siku hiyo ndipo Igor alipoamua career ya maisha yake. Aliishi St Petersburg( kabla mji haujajitenga kama saiv) miaka 3 ndani ya Naval college ( jeshi la majini) wakati huohuo akiwa mwanafunzi pale Mechanical Engineering College of the Polytechnic Institute mjini Kiev.
Igor alisafiri kwenda Paris kusoma uinjinia ambapo alikutana na wataalamu wa mambo ya anga kama Louis Bleriot,na badaye alirudi nyumbani na kuanza majaribio ya kutengeneza Helicopter yake ya kwanza.
Hivyo alitengeneza Helicopter ya kwanza 1909, ya pili akatengeneza 1910 ambapo sasa pamoja na kuwepo 15-horse power, ya kwanza haikuruka na ya pili iliruka tena aliiendesha yeye na ni umbali mfupi, na pia ya kwanza ilishindwa ku-sustain ile weight ya rubani ndy mana ikashindwa.
Hapo juu kwenye picha ni Igor S akiwa na helicopter yake ya pili aliyotengeneza mwaka 1910.
1913 alitengeneza nyingine ambayo ni 50 horsepower engine na alibaki hewani zaidi ya lisaa kwa altitude ya 450m, na alifanya safari fupi ndani ya nchi hiyo.
Hii ni picha ya mwaka 1913 na alipigwa wakati akiwa amesimama mbele ya model yake mpya ya aircraft ila picha ya jumla haikuonekana vizuri.
Na hii ilioelekea kupata leseni na pia tuzo kwa kazi yake👇👇👇👇
Basi March 30 1919, mwamba alihamia Newyork marekani. Kuhama kwake Russia kulitokana na mapinduzi yaliyokuwepo kule (tulisoma sekondori kuhusu Russia Revolution) ambapo kila officer au injinia au tuseme msomi walitaka kumkamata na kumuua hivyo yy hakutaka hilo.
Akiwa US kama mwalimu wa hesabu au lecturer7, alitafuta eneo atakapofungua kiwanda chake na rafiki yake alimpa shamba na kiwanda hiko aliita Sikorsky Aero Engineering Corp,hali ya uchumi ilikua ngumu ndipo rafiki yake mwingine Sergei Rachmaninoff aliwekeza $50000 ili ishu zikae sawa. 1924 alitengeneza aircraft ya kwanza na iliruka, baadaye 1928 akawa
citizen wa US, alitengeneza pia aircraft zingn baadaye kama fyling boats zilizopita Atlantic na Pasicif oceans (1929-1937).
Yan hizi hapa chini 👇👇👇
Story ni ndefu, ila rasmi kuanzia 1938 alianza kutengeneza helicopter (practical one), na akiwa kama Engineering Manager wa Vought-Sikorsky Division of United Aircraft Corporation, aliweza shawishi viongozi wa US kuhusu mpango wake.
Hatimaye september 14 1939, alimaliza mission yake na chuma alichotengeneza kilifanikiwa kama alivyotarajia. Helicopter hii aliipa jina la VS-300 (V-Vogous, S-Sirkorsky) na picha hii hapa chini inaonyesha first flight ya hiyo helicopter, mwaka 1939 september 14.
Hapa chini pia ilikua ni public demostration flight, mwaka huohuo 1939.
Hapa akitest mambo👇👇👇
VS-300 ikiwa hewani 👇👇👇
Naam,👇👇
Improvements👇👇👇
👇👇 Huyu ndiyo yule jamaa ake walikutana Paris alipoenda kujiendeleza kielem kuhusu uinjia
Dah Wakuu ninaeza andika mengi sana kuhusu jinsi alivyotengeneza Helicopter na picha zake pia kuweko ila tuishie hapa.
NB: Huyu siyo wa kwanza kutengeneza chombo hicho ila yeye alikua wa tofauti kuliko wengine na ndiyo Helicopter zote zimetengenezwa kupitia innovation yake. Wako wengine walijaribu ila walishindwa.
Baadhi yao ni hawa hapa👇👇👇
1.
Huyu mwamba anaitwa Paul Cornu na hapa ilikua mwaka 1907 kwenye helicopter yake ya kwanza, Ukimwangalia ni amekaa kati ya rotors mbili ambapo zilizunguka uelekeo tofauti yan in opposite direction ili ku-cancel torque. Hii ilikua ni helicopter ya kwanza kunyanyuka kwa kutumia rotor blades badala ya wings
2.
Huyu anaitwa Louis Breguet alitengeneza yake pia mwaka 1907 na ni full scale na pia pilot aliweza kuitumia ila sasa haikua na uwezo wa kua controlled yani namaanisha haikua na 'means of controll'.
3.
Huyu ni Emile Berliner wa ujerumani mwaka 1908
4.
Huyu ni J.C.H Ellehammer mwaka 1912 pale Dernmak na haikuruka zaidi ya 1ft.
Na wengineo wengi!
Basi kila safari ina mwanzo na mwisho wake.
26 Oct 1972 (aged 83)Easton, Fairfield County, Connecticut, USA ndipo alifariki.
|