GALLERY: What are some rare pictures that you have never seen? Here are some of them...

GALLERY: What are some rare pictures that you have never seen? Here are some of them...

IMG_20220116_193301.jpg


Huyu ni Hans Georg Henke akionekana akilia baada ya kuchukuliwa mateka na jeshi la Ujerumani maana Askari wengi wa Kijerumani waliuwawa wakati wa vita, Sasa mpango ni kuchukua vijana na kuwapelekea jeshini.

Picha hii ilipigwa mwaka 1945 na Askari wa Jeshi Marekani na Hans (kwenye picha) alikua na umri wa miaka 15 tu. Wazazi wake wote wawili walifariki wakati wa vita na yeye alibaki hai sababu alikubali kwenda jeshini.
 
Naomba mwenye kujua story ya kina kabisa ya Chacha Wangwe kuzaliwa mpaka kifo
 
. Dr June Almeida: Mwanamke aliyegundua Corona virus kwa mara ya kwanza.
View attachment 1424269
Mama huyu ni mtu wa scotland, aligundua virusi vya corona mwaka 1964 alipokua maabara ndani ya hospitali ya St thomas mjini London.
Akiwa na miaka 16, aliacha kusoma baada ya kupata kazi kama 'histopathology laboratory technician' (Histopathy is the study and diagnosis of tissue diseases and involves examining cells and tissue under a microscope, according to the Royal College of Pathologists) ila baadaye aliamua kwenda London kujiendeleza kielimu.

Muonekano wa Corona virus kupitia microscope ulikua hiv kwa mara ya kwanza 1964..[emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1424280
View attachment 1424281

Alihama England na kuelekea canada kwa kazi zake. Baadaye alirudi tena England palepale St Thoman hospital ambapo kama unakumbuka hii ndiyo hospitali iliyotumika kumuuguza Boris Johnson waziri mkuu wa uingereza wakati kapata maambukizi ya Covid-19.
Katikati ya miaka ya 80 akiwa hapo London, alisaidia kupata picha za HIV.

Dr June almeida alifariki mwaka 2007 kwa heart attack (london hapo hapo) akiwa na miaka 77. Alizaliwa october 5 1930.
View attachment 1424285
Covid 19 na hiyo ya 1960' imekaaje hii
 
Lina Marcela Medina de Jurado, Youngest confirmed mother in Medical History.

Lina Medina ni Binti aliyezaliwa mji wa Paurage nchini Peru September 23, 1933. Binti huyu akiwa na miaka 5, miezi 7 na siku 21 yaani Mwezi wa 5, 24, mwaka 1939, alijifungua mtoto wake wa kwanza ambapo alipopimwa ilionekana uzito wa mtoto ni Kilo 2.7. Hii ina maana uja uzito aliupata akiwa na umri wa miaka minne (4) tu.
Picha hii hapa chini ni muonekano wake akiwa mja mzito.
IMG_20220220_132557.jpg


Kwa kipindi kile haikujulikana ni nani anahusika na uja uzito wake, hivyo baba yake mzazi Mzee Tiburelo Medina alihisiwa kua huenda alim-baka bintiye ila baadaye aliachiwa kutokana na kukosekana Kwa ushahidi wa tukio Hilo. Mkewe alikua akiitwa Victoria Losea.



Chini hapa ni baadhi ya picha za Lina Medina akiwa na mwanaye wa kiume ambaye alipewa jina la Gerardo. Gerardo alikuwa ni Daktari wa kwanza kujua Kua Lina ana uja uzito na ikabidi amchukue kumpeleka Kwa wataalamu zaidi kwaajili ya kufanyiwa upasuaji (C-section).

  • Akiwa hospitali pamoja na Nurse baada ya kujifungua
IMG_20220220_134845.jpg

  • Hapa ni akiwa na Doctor Gerardo, aliyejua na kuthibitisha kua unene na Hali ya Lina inatokana na Uja uzito
IMG_20220220_135109.jpg

  • Akiwa na mwanaye
IMG_20220220_135419.jpg

  • Lina na Gerardo mitaani
IMG_20220220_135558.jpg

IMG_20220220_135542.jpg

IMG_20220220_141726.jpg


Je, Gerardo alijua kua Lina ndiye mama yake mzazi?
Ukweli ni kwamba, katika kipindi Cha awali Cha ukuaji wa Gerardo hakuelezwa waziwazi kua Lina ndiye Mama yake Bali aliambiwa ni dada yake. Gerardo alipofikisha umri wa miaka 10 ndipo alipoambiwa rasmi kua Lina ni Mama yake mzazi.
  • Picha hii hapa chini ni Lina pamoja na Gerardo, Gerardo ni huyo wa upande wa kushoto
IMG_20220220_180039.jpg


  • Picha hii hapa chini ni Lina akiwa anaenda kazini kama secretary wa Clinic alipojifungulia Gerardo, fedha aliyopata alimsomeshea mwanaye na kiasi kingine alijiendeleza binafsi. Hii picha ni ya mwaka 1969.
IMG_20220220_181732.jpg

Je, Lina aliolewa katika maisha yake?
Ndiyo aliolewa. Mwanzoni mwa miaka ya 1970 aliolewa na jamaa aliyeitwa Raul Jurado na Lina akafanikiwa kupata mtoto wa pili mwaka 1972.
  • Picha hii hapa ni Lina pamoja na Mmewe Raul mwaka 1972
IMG_20220220_174756.jpg



Basi mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka 40, Gerardo alifariki dunia Kwa tatizo linaloitwa Bone marrow disease (kiswahili rasmi Sifahamu).


Je, Kwa Sasa Lina Medina Yuko hai?
Jibu ni ndiyo, Lina Medina Yuko hai na anaishi nchini Peru, maisha yake ni ya kawaida sana na amefanya historia ya maisha kua ni Siri Kwani hata Mwaka 2002 alikataa kufanya mahojiano na waandishi wa habari kumuhusu kama ambavyo amekua akifanya kipindi Cha nyuma.
Picha yake hapa chini ni yeye na ilikua mwaka 2018.
IMG_20220220_183309.jpg


MWisho.
 
Nmsikitika story ya lina...sijui ni nani huyo aliemu abuse akiwa mdogo hivyo na kumsababishia kupata kuzaa kwa kipindi hicho.
Kukataa kwake kuongeleea hilo swala kuna onesha bado ana maumivu makali.
 
Nmsikitika story ya lina...sijui ni nani huyo aliemu abuse akiwa mdogo hivyo na kumsababishia kupata kuzaa kwa kipindi hicho.
Kukataa kwake kuongeleea hilo swala kuna onesha bado ana maumivu makali.
Lakini mkuu mbona ipo kama illusion hii kitu
Binti wa miaka 4 awezaje pata mimba while hata kupevuka bado
Au ndio yale ya wafia dini kwamba mbimba ni uwezo wa holly spirit ambae mmi na shindwa pata majibu logically
 
Back
Top Bottom