Maafisa wa ngazi za jeshini wa umoja kiSoviet wakitazama mabaki ya Vladimir Komarov ambaye alianguka tokea angani April 24 mwaka 1967.
View attachment 1594890
Vladmir Komarov alikua ni mmoja wa watu wenye ujuzi katika kurusha vyombo angani yaani spaceflight, na alizaliwa 16 march 1927 nchini Russia.
View attachment 1594914
Mazingira ya kifo chake yaliyotokea kipindi umoja ule wa kiSoviet umepanga kusherekea miaka 50 tangu msingi wake na serikali ya kipindi kile chini ya Leonid Brezhnev, walipanga kusherekea kwa namna ya pekee.
Ni ipi? Ni kupitia kutengeneza space vehicles 2 (Space Capsule) ambazo baada ya kufika angani, yani kwenye outer space, zitaenda mwendo sambamba yani Orbital docking na kisha aliyeko ndani ya chombo kimoja atahama na kuhamia chombo kingine, wakiwa angani wote mda huo.
Space vehicle ya kwanza iliitwa Soyuz 1 ambayo ndiyo Vladimir aliondoka nayo kwa siku ya kwanza na ya pili iliitwa Soyuz 2 ambayo ndiyo ingeondoka siku ya pili yake ikiwa na watu wawili ambapo sasa zitakutana na zitaenda sambamba yani orbital docking halafu Vladimir atahama kupitia kutambaa yani crawling kutoka aliko na ataenda kwenye hicho chombo kingine Soyuz 2 halafu ndicho atakachorudi nacho duniani.
Sasa Vladimir alichaguliwa huku mbadala wake akiwa ni Yuri Gagarin ambaye wamekua wote tangu udogoni na walifanya mambo mengi pamoja kama uwindaji n.k
View attachment 1594936
Yuri G ni huyo wa upande wa kushoto.
Sasa kila mmoja aliyehusika kutengeneza kile chombo walijua hakiko salama kwaajili ya hiyo safari na huenda kifo kikawepo. Sasa Komarov hakutaka rafiki yake aende na hicho chombo kwani alijua fika kua hatorudi akiwa hai na lazima atakufa. Hivyo ndivyo alivyoamua.
Kadri siku zilivyokua zinasogea, wataalam walibaini matatizo ya kiufundi 203 na jamaa hakujali kwasababu ilikua ni lazima kwa amri lasivyo Yuri ataenda na yey hataki.
Sasa Komarov aliondoka na hicho chombo na dakika 8 badaye alikua kwenye orbit tayari, sasa kashehe ikaanza kwenye Solar Panels kufunguka ambazo hua zinapokea mwanga wa jua na kutengenza umeme, na kadri muda ukivyoenda ndivyo shida zikazidi.
Komarov ikabidi ajitahidi kubadilisha orbit aliyokuwepo ili nafuu iwepo ila haikufanikiwa. Alivyotaka kufanya usahihisho ndivyo ambavyo kile chombo kilizunguka dunia kwa spidi isiyo ya kawaida.
Ndani ya masaa 5 alijaribu bila mafanikio kufanya astro-orientation, kukirudisha kwenye njia iliyotakiwa na kwa shida aliyopata ilifanya afanye trip 2 zaidi kuzunguka dunia na kufikia 18.
Maafisa wa anga baada ya kuona hivyo ikabidi waghairi mpango wao wa kutuma Soyuz 2 ambayo ndiyo ilikua ifanye orbital docking na Komarov ahame kwenye Soyuz 1 aje 2 hivyo ikabidi wapambane na yeye pia waweze kurudisha chombo duniani na Komarov alifanikiwa kuingia kwenye earth's atmosphere.
Wakati sasa anarudi huku akiwa na spidi kubwa, ilibidi atumie parachute ili atue salama na pia spidi ipungue ya hicho chombo. Ile Drogue parachute (hua zinatumika kupunguza spidi kwa vitu vinavyotembea angani na pilot anaweza itumia pia) haikufunguka na hata zile za akiba nazo hazikufunguka ipasavyo.
Kwa spidi kubwa sana huku kikionyesha dalili za kuungua, Komarov alianguka na hicho chombo na alifariki dunia.
Baadhi ya picha za sehemu alipodondokea ni kama hivi hapa chini:
View attachment 1595004
View attachment 1595005
Hapa chini ni maafisa wa jeshi ngazi za juu waliwasili
View attachment 1595006
View attachment 1595007
View attachment 1595008
View attachment 1595009
Mwisho: Inaaminika kifo cha Vladimir Komarov kilipangwa hasa ukizingatia tangu awali space capsule haikua sawa ila sababu ya anniversary ilibidi itokee.
Space Capsule ni nini?
Hiki ni kifaa ambacho kina uwezo wa kufanya safari za anga kwenda kwenye outer space na bado kikarudi duniani. Hiki ni tofauti na satellite na kinaizunguka dunia na bado taarifa zinapatikana kama kawaida.
Kiko hivi:
View attachment 1595023
View attachment 1595021
View attachment 1595022