Lina Marcela Medina de Jurado, Youngest confirmed mother in Medical History.
Lina Medina ni Binti aliyezaliwa mji wa Paurage nchini Peru September 23, 1933. Binti huyu akiwa na miaka 5, miezi 7 na siku 21 yaani Mwezi wa 5, 24, mwaka 1939, alijifungua mtoto wake wa kwanza ambapo alipopimwa ilionekana uzito wa mtoto ni Kilo 2.7. Hii ina maana uja uzito aliupata akiwa na umri wa miaka minne (4) tu.
Picha hii hapa chini ni muonekano wake akiwa mja mzito.
Kwa kipindi kile haikujulikana ni nani anahusika na uja uzito wake, hivyo baba yake mzazi Mzee Tiburelo Medina alihisiwa kua huenda alim-baka bintiye ila baadaye aliachiwa kutokana na kukosekana Kwa ushahidi wa tukio Hilo. Mkewe alikua akiitwa Victoria Losea.
Chini hapa ni baadhi ya picha za Lina Medina akiwa na mwanaye wa kiume ambaye alipewa jina la Gerardo. Gerardo alikuwa ni Daktari wa kwanza kujua Kua Lina ana uja uzito na ikabidi amchukue kumpeleka Kwa wataalamu zaidi kwaajili ya kufanyiwa upasuaji
(C-section).
- Akiwa hospitali pamoja na Nurse baada ya kujifungua
- Hapa ni akiwa na Doctor Gerardo, aliyejua na kuthibitisha kua unene na Hali ya Lina inatokana na Uja uzito
Je, Gerardo alijua kua Lina ndiye mama yake mzazi?
Ukweli ni kwamba, katika kipindi Cha awali Cha ukuaji wa Gerardo hakuelezwa waziwazi kua Lina ndiye Mama yake Bali aliambiwa ni dada yake. Gerardo alipofikisha umri wa miaka 10 ndipo alipoambiwa rasmi kua Lina ni Mama yake mzazi.
- Picha hii hapa chini ni Lina pamoja na Gerardo, Gerardo ni huyo wa upande wa kushoto
- Picha hii hapa chini ni Lina akiwa anaenda kazini kama secretary wa Clinic alipojifungulia Gerardo, fedha aliyopata alimsomeshea mwanaye na kiasi kingine alijiendeleza binafsi. Hii picha ni ya mwaka 1969.
Je, Lina aliolewa katika maisha yake?
Ndiyo aliolewa. Mwanzoni mwa miaka ya 1970 aliolewa na jamaa aliyeitwa Raul Jurado na Lina akafanikiwa kupata mtoto wa pili mwaka 1972.
- Picha hii hapa ni Lina pamoja na Mmewe Raul mwaka 1972
Basi mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka 40, Gerardo alifariki dunia Kwa tatizo linaloitwa
Bone marrow disease (
kiswahili rasmi Sifahamu).
Je, Kwa Sasa Lina Medina Yuko hai?
Jibu ni ndiyo, Lina Medina Yuko hai na anaishi nchini Peru, maisha yake ni ya kawaida sana na amefanya historia ya maisha kua ni Siri Kwani hata Mwaka 2002 alikataa kufanya mahojiano na waandishi wa habari kumuhusu kama ambavyo amekua akifanya kipindi Cha nyuma.
Picha yake hapa chini ni yeye na ilikua mwaka 2018.
MWisho.