PreGE2025 Gambo afuturisha Arusha, asema anajivunia kuwa sehemu ya shughuli hiyo ya kujenga jamii iliyojaa huruma na upendo

PreGE2025 Gambo afuturisha Arusha, asema anajivunia kuwa sehemu ya shughuli hiyo ya kujenga jamii iliyojaa huruma na upendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wakuu naona Iftari zinaendelea kwa wingi

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, ameandaa Iftar maalum kwaajili ya watoto yatima na viongozi wa dini, iliyofanyika jana Machi 22, 2025.

Hafla hiyo ya Iftar iliwaleta pamoja watoto yatima waishio katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuonesha mshikamano na upendo katika jamii.
1742721548632.png

Akizungumza katika hafla hiyo, Gambo amesema kuwa Iftar hiyo inalenga kutoa msaada na faraja kwa watoto yatima, pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya viongozi wa dini na wananchi.

Ameongeza kuwa kipindi cha Ramadhani ni wakati wa kujitolea na kusaidiana, na kwamba anajivunia kuwa sehemu ya shughuli hiyo ya kujenga jamii iliyojaa huruma na upendo.

Kwa upande wao, viongozi wa dini walioshiriki walishukuru kwa mchango wa Gambo na kumpongeza kwa kuendeleza utamaduni wa kusaidia watoto yatima, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuungana na kusaidiana, hasa katika nyakati za majanga na changamoto.

Iftar hiyo ilihudhuriwa na mamia ya watu, wakiwemo watoto yatima, wananchi na viongozi wa dini, huku ikijumuisha dua na sala kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amani pamoja na mafanikio ya taifa.
1742721656189.png
 
Huyu kazi anayo! Mbeleko ya mwendazake ya kumnusuru haipo, mtoto pendwa akitangaza nia tu hapo Arusha huyu anaelekea veta
 
Back
Top Bottom