PreGE2025 Gambo akubali yaishe. Aomba radhi na kufuta kauli yake

PreGE2025 Gambo akubali yaishe. Aomba radhi na kufuta kauli yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Gambo alitaka kumchezea mkwe? Akafinywa chaap kabadili maneno lol.

Huyu ubunge hapati tena, woiiiiih
 
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa leo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kuna ombi la Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo anataka kusema jambo.

Amesema kwa kutumia kanuni namba 70 ya kanuni za Kudumu za Bunge Tolea la Februari 2023 anampa nafasi ya kusema ambayo inasema kutokusema uongo Bungeni.

Soma, Pia: Gambo aibua tuhuma za ufisadi wa mabilioni Arusha, Spika Tulia amwagiza Mchengerwa kuandaa ripoti iwasilishwe Bungeni

Mapema leo Jumatano Aprili 23, 2025, Spika aliagiza Mbunge huyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohamed Mchengerwa wakasikilizwe na Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya kuwa na mabisho kuhusu tuhuma ambazo zilikuwa zimeibuliwa kutoka Arusha.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Mheshimiwa Spika, utakumbuka ilitokea sintofahamu leo asubuhi. Baada ya kukaa na kutafakari nimeona niombe radhi," amesema Gambo.
Gambo amesema katika kipindi cha asubuhi ulitokea aliouita mtifuano ambao hakutaja nini maana yake.

Mbunge huyo amesema hawezi kuendelea zaidi kwani makofi ya wabunge yameonyesha kuwa wamemsamehe hivyo anaomba aishie hapo asije akaharibu.
Angesimamia tu msimamo. Maana hii nchi wamefanya kama ya familia
 
Gambo alikuwa anawaza nini kuleta kamdomo kwa kifua kipana. Hajui kanuni za mchezo? Na ubunge unaweza ukawa umeahaota mbawa.
Wakati wa uongozi wa JPM, role model wa Gambo, Ali Happi, Chalamila na Sabaya alikuwa ni Makonda. Makonda alikuwa anawasogeza karibu kwa JPM na wakawa ni ma-RC untouchable, kiasi Ali Happi, Makonda mwenyewe na Chalamila waligoma kwenda Tamisemi baada ya kuitwa kwenye kikao cha nidhamu na boss wao, Waziri wa Tamisemi, wakati huo akiwa ni Jaffo. Gambo aliwahi kuitwa, akafika Wizarani akiwa amevaa kofia kidharauu.

Baada ya Chalamila kuwapiga viboko wanafunzi kule Mbeya, Jaffo alimuita Dodoma lakini, JPM alipita Mbeya na akasema Chalamila umefanya vyema, nione mtu wa kukugusa, Jaffo akaishia kucheka tu, wito wa kuitwa TAmisemi ukafa hapohapo

Wakati huu wa utawala wa SSH, Gambo anaona amekuwa mkubwa sasa na anaamua kupambana na role model wake (Makonda). Ndio unatimia ule usemi wa kinyago hakiwezi kumtisha mchongaji.
 
Gambo ni Kiongozi mzuri:
Ila anapenda sana Bifu:
Mku wa mkoa Arusha, Bifu na Mbunge Lema:
Mbunge arusha, Bifu na Makonda
Bungeni, Bifu na Mchengerwa:

Hao ambao wako naye chama kimoja kama wana kasoro ni kwanini haendi kuongea nao binafsi au katika vikao vya Chama:
 
Tulisema na tutaendelea kusema HAKUNA bunge pale ni kikao cha chama (fisiem)
KAZI ni kipimo cha utu
 
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa leo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kuna ombi la Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo anataka kusema jambo.

Amesema kwa kutumia kanuni namba 70 ya kanuni za Kudumu za Bunge Tolea la Februari 2023 anampa nafasi ya kusema ambayo inasema kutokusema uongo Bungeni.

Soma, Pia: Gambo aibua tuhuma za ufisadi wa mabilioni Arusha, Spika Tulia amwagiza Mchengerwa kuandaa ripoti iwasilishwe Bungeni

Mapema leo Jumatano Aprili 23, 2025, Spika aliagiza Mbunge huyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohamed Mchengerwa wakasikilizwe na Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya kuwa na mabisho kuhusu tuhuma ambazo zilikuwa zimeibuliwa kutoka Arusha.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Mheshimiwa Spika, utakumbuka ilitokea sintofahamu leo asubuhi. Baada ya kukaa na kutafakari nimeona niombe radhi," amesema Gambo.
Gambo amesema katika kipindi cha asubuhi ulitokea aliouita mtifuano ambao hakutaja nini maana yake.

Mbunge huyo amesema hawezi kuendelea zaidi kwani makofi ya wabunge yameonyesha kuwa wamemsamehe hivyo anaomba aishie hapo asije akaharibu.
Kusanyiko la chawa wa mama.
 
Gambo alitaka kumchezea mkwe? Akafinywa chaap kabadili maneno lol.

Huyu ubunge hapati tena, woiiiiih
Na ubunge wa Arusha mjini asahau kabisa Nyamitako ameshamaliza kazi anamgojea kuapishwa tu November.
 
Kipindi cha dhalimu magu alikuwa anawaletea wapinzani sifa za kikuda mkawa mnamuona mzalendo. Haya huyo hapo katema bungo, mnaishia kumnanga. Au ndio mambo ya kutumika kama condom?
Matusi nayajua zaidi yako kama unataka tutukanane sawa mkuu.
 
Tukana mkuu, mimi matusi siyawezi kama ww, ila hapa utafurahia show.
Nataka nikutukane live. Upo wapi nije? Mimi nipo hapa Kisutu nataka kuelekea Obay.
 
Kila tukikaa vikao hapa kazini najiona mimi ni kaka Gambo maana kikao hakiishi bila kugombana na watu wote kwenye kikao ila nahisi ni wivu wao tu .
Mei mosi ile pale soon mtumishi bora wa mkoa .Nasubiri kwa hamu .
 
Back
Top Bottom