Gambosi (Gamboshi) na Nadharia ya uchawi

Gambosi (Gamboshi) na Nadharia ya uchawi

Gamboshi ndio makao makuu ya uchawi Tza,ni mji Mkubwa sana usiku una ghorofa 120 una treni ya kisasa ya umeme hadi bamuda triangle.
Gamboshi ulianzishwa na Hitler akauficha isionekane live
Hitler yule mjerumani au yupo mbongo
 
Gamboshi/Gambosi na Nadharia ya uchawi.

Kijiji cha Gambosi(Gamboshi) ni moja wapo ya kijiji ndani ya kata ya Gambosi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Jina halisi la kijiji hicho ni Gambosi wala si Gamboshi kama wengi ambavyo hutamka hivyo kiuhalisia kijiji hicho si GAMBOSHI Bali ni GAMBOSI.

Gambosi huitwa Gamboshi kutokana na neno hilo kukaa mdomoni mwa watu ambalo ni Rahisi kutamkika, pia inasemekana kuwa kwa wasukuma wa mwamza ndio huita Gamboshi lakini Wasukuma wa Shinyanga na Simiyu wao huita Gambosi sababu Wasukuma asili ya kinyantunzu Baadhi ya maneno hushindwa kutamka mfano Shi wao hutamka Si.
Jina halisi la kijiji hicho ni kutokana na jina la mzee aliye kuwa mkazi wa kijiji hicho aitwaye Gambosi aliye fariki zaidi ya miaka 100 iliyo pita.

Gamboshi/Gambosi imepakana na maeneo mengine yaani vijiji vingi kama vile Banemhi | Dutwa | Gibishi | Gilya | Ihusi | Ikungulyabashashi | Itubukilo | Kasoli | Kilalo | Masewa | Matongo | Mwadobana | Mwasubuya | Mwaubingi | Mwaumatondo | Ngulyati | Nkindwabiye | Nkololo | Sakwe | Sapiwi

Video chini inaonyesha baadhi ya mahojiano yaliyo fanywa kijijini hapo ambapo Mkazi wa kijiji hicho Mzee Masuke Ngusa ameeleza juu ya nadharia hiyo kuwa hapo kuna eneo ambalo Husadikika Wachawi nchi nzima hukusanyika kila mwaka kufanya matambiko kijijini hapo na nadharia ya kwamba kijiji hicho ni makao makuu ya wachawi ndio hujionyesha.

Pia hatukuishia hapo moja ya kijani mkazi wa Gambosi Paul Rawson nae alieleza kuwa mwanzo ndipo uchawi ulikuwepo eneo hilo na kusema wachawi walisababisha kupoteza moja ya mzazi wake, pia Paul aliongezea kusema na kuwataja nguli wa kisukuma kama Ng'wana malundi kuwa ndiyo walikuwa na dawa kipindi hicho lakini kwa sasa uchawi umeisha kijijini hapo na maisha yanaendelea kama kawaida.

Baada ya hapo Mtendaji wa kijiji cha Gambosi Charo charles alisema uchawi wa Gamboshi ni kama uchawi uliyopo katika maeneo mengine nchini pia aliwatoa hofu watu kuwa kijiji hicho si makao ya uchawi kama wengine wanavyo Zani alisema mtendaji huyo.

Ukweli ni kwamba Kijiji cha Gambosi na nadharia ya uchawi hii huchukuliwa kama imani ya Mtu/Watu hivyo mpaka sasa kuna watu wanaamini Gamboshi ni makao makuu ya wachawi na wengine kupinga hilo hivyo tutaendelea kuchunguza Nadharia ya uchawi kijijini hapo.




Karibuni nitarudi kijijini hapo kuendelea na utafiti.

Wewe beza tu huku kwetu Gamboshi, utakuja na miguu miwili ukiwa na bahati utaondoka na miguu minne!
Nipitie hapa Ngulyati ukienda tena.😜
 
Wewe beza tu huku kwetu Gamboshi, utakuja na miguu miwili ukiwa na bahati utsondoka na miguu minne!
Nipitie hapa Ngulyati ukienda tena.😜
Sawa mkuu upo hapo jirani na gambosi ili uwe mwenyeji wangu?
 
Made in gamboshi

ECv-mqdXsAELA6O.jpg


hqdefault.jpg
 
Back
Top Bottom