Game ya mziki ilipofikia (huge IQ only)

eastmea

Senior Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
159
Reaction score
133
Ndugu, jamaaa na marafiki pamoja na wadau mbalimbali wa huu mziki wa bongo fleva nnawaomba tusaidizane kulichambua hili game la bongo fleva.
Mtazamo wangu: game la bongo fleva linazidi kuwa gumu kadri siku zinavyozidi kwenda mbele hii ni kutokana na jinsi ambavyo wadau wa mziki jinsi wanavyoliendesha game, game la bongo fleva limegawanyika katika makundi mbalimbali mfano team clouds ambao wapo pamoja na team kiba pia kuna kundi jingine ambao ni team WCB ,mgawanyiko katika haya makundi kinafanya wasanii wengine wachukiliwe kawaida na mashabiki mfano msanii ambaye hausiani na haya makundi akifanya show yake mashabiki hawatokei kussuport kwa wingi. Lakin mfano wasanii ambao wapo katika mgawanyiko wa haya makundi wakifanya show mashabiki wanatokea kwa wingi mfano kingkiba,diamond, harmonize,aslay,mbosso,rayvanny,nandy, lavalava nk pia huu mgawanyiko umefanya wasanii ambao hawausiani na haya makundi kutosikika kwa kazi zao hii ni kutokana na mashabiki wapo busy na watu wao wanaowasapot.
Pia hizi team kumefanya kuwepo
Wasanii ambao hawausiani na hizi team hukosa sapot hata kama wimbo ni mzur lakin wasanii ambao wapo kwenye hizi team wakitoa wimbo hata kama ni mbaya mashabiki watasapot na kuufanya kuwa wimbo pendwa
Pia Game ya mziki sahivi emegawanyika katika makundi mawili yenye nguvu kwa sasa amboyo ni clouds vs WCB.haya makundi yanawaathili wote wawili mfano clouds ni media iliyojijengea mizizi katika habari ya mawasiliano ambapo wanapatikana katika nchi nzima kwenye swala zima la radio,hakuna ambaye afahamu kuwa clouds hawapigi nyimbo za WCB ambapo inawapunguzia nyimbo zao kutosikika kwa haraka katika maeneo husika ambapo clouds wanapatikana pia hakuna asiyefahamu kuwa WCB ni team ambayo imejijengea mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania ambapo imepelekea mashabiki wake kutosikiliza team media ya clouds ambapo mashabiki wamehamia katika media mbalimbali especially times FM
Pia mwaka huu tutashuhudia matamasha mawili ambayo ni fiesta vs wasafi festival kwa upande wa matamasha ndo utaenda kudhihilisha nani ana mashabiki wengi hii atajijidhilisha katika mahudhulio ya matamasha hayo kwa sababu mashabiki wa WCB hawatahudhulia katika tamasha la fiesta pia hivyohivyo mashabiki wa fiesta hawatahudhulis katika tamasha la wasafi festival hii ni kutokana na chuki ambazo wadau wakubwa wa mziki wamewajengea mashabiki
Ushauri wangu:: wadau wa mziki inatakiwa waungane katika kuufanya mziki wa bongo fleva kuwa ndo mziki wa afrika kama walivyoufanya kuwa mziki wa afrika mashariki inatakiwa waige kwa wenzetu wamarekani na wanigeria ambao wameungana hata kama kuna beef Bali litakuwa haliusiani na media litakuwa msanii kwa msanii
 
Kikubwa wasanii walipwe vizuri tu!
Ili waache malalamiko kama wamapunjwa na clouds!

Naamini ushindani huu utaleta chachu kwa wasanii kuona wapi malipo yako vizuri
 
Muziki umeama na umeamia kwenye social media.. Anaefikiri bado anaweza kutawala sanaa sababu ana radio pendwa basi anajidanganya.. Huu ni mwanzo tu yajayo yanafuraisha.
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91] game imekuwa ngumu
 
Kikubwa wasanii walipwe vizuri tu!
Ili waache malalamiko kama wamapunjwa na clouds!

Naamini ushindani huu utaleta chachu kwa wasanii kuona wapi malipo yako vizuri
Kabisa
 
Muziki umeama na umeamia kwenye social media.. Anaefikiri bado anaweza kutawala sanaa sababu ana radio pendwa basi anajidanganya.. Huu ni mwanzo tu yajayo yanafuraisha.
Ni kweli social media zina nguvu kipindi hiki..lakini radio bado zina mchango wake

Marekani wasanii wenyewe wanataka airtime hot97,wakati internet kwao ni kama maji tu,sasa bongo kwa nini redio zisiwe na mchango??
 
Ni kweli radio ina mchango mkubwa sana kwa msanii,especially kwenye kuzungumziwa story za msanii,na hiyo ni moja ya kitu kinachokosekana kwenye social media, msanii kuongelewa kwenye radio ni mhimu sana kuliko hata kuplay nyimbo..
 
Darasa alikuwa upande gani clouds au team kiba?

Maya sama yupo upande gani clouds au team kiba?
 
Watakao piga hela ni wale wasio na kambi na wenye nyimbo kali. Utaitwa ukapige shoo za e FM, mawingu, na wasafi.
Tunataka makundi makundi kama haya yawe mengi zaidi ila tuu kuwe na mikataba inayipitiwa na basata.
 
Ningekuwa Efm ningezisha tamasha ningeliita STRICTLY HIPHOP hapa ningekusanya wakali wa hiphop na kuafanya nao matamasha kukingana na upepo. Why ? No one is doing that. Na hii Inge compensate radha inayokosekana ya mkali was rhymes na hip hop summit lazima ingepata wapenzi tu piga ua
 
tupo bize na Jibebe , Kwangwaru , ilike it, mes selekta , Vanessa na nyimbo staili hiyo . Ukiweka tamasha hilo utapata watu 10 au labda aliweke Diamond maana Kiba nae anavyozidi kukaa kimya anazidi kupoteza ushawishi wake
 
Kila kitu ni promo Mzee. Dogo mfaume haja hit kama sharomwamba. Msagasumu haja hit kama sharomwamba...Mdogo haki the same unajua tifauti ni nini ? Promo mzee promo
 
Nilipoona umeeandika "Huge IQ Only" nikataka kuukwepa huu uzi lkn kumbe ulichoandika wala hakiitaji akili kubwa. Ulitaka kututenga bure wenye IQ ndogo
 
Nilipoona umeeandika "Huge IQ Only" nikataka kuukwepa huu uzi lkn kumbe ulichoandika wala hakiitaji akili kubwa. Ulitaka kututenga bure wenye IQ ndogo
Oky mkuu basi hebu nipe maoni yako juu ya kile nilichoandika hapo juu
 
Watakao piga hela ni wale wasio na kambi na wenye nyimbo kali. Utaitwa ukapige shoo za e FM, mawingu, na wasafi.
Tunataka makundi makundi kama haya yawe mengi zaidi ila tuu kuwe na mikataba inayipitiwa na basata.
Mkuu inapaswa utambue haya makundi mawili ndo yananguvu kwenye swala zima la mziki tofauti na hao Efm
 
Jana nilikuwa naangalia interview moja ya Fid Q, kimsingi alisema hivyo hivyo alivyosema mleta maada kuhusu makundi kufanya wasanii wazuri wasio katika makundi kutosikika.
 
Jana nilikuwa naangalia interview moja ya Fid Q, kimsingi alisema hivyo hivyo alivyosema mleta maada kuhusu makundi kufanya wasanii wazuri wasio katika makundi kutosikika.
Mara zote ukiwa vugu vugu unakuwa huaminiki, siyo lazima ujiunge na wasafi au clouds ile kuonekana tu unamtazamo wa upande gani inatosha. Wasanii wengi ni wanafiki sana hivyo hawapendi kuonekana wapo upande gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…