Gamers only: FIFA vs PES ipi unaikubali?

fifa ndo kali,pes limekaa kitoto sana
 
mizuno,
Hiyo mipira kama sikosei inaitwa though ball, FIFA 14 nimefungwa sana na mpinzani kwa hayo magoli, kuna kipindi nilihisi jamaa kaniwekea patch ila baadae kwenye upande tactics kuna kitu kinaitwa kama Man Marking. Yaani kwa mfano Benzema unamuekea beki ambae muda mwingi anakuwa nae na pia katika defense yako umeweke wakabe kwa njia ya offiside trap na kipindi ambacho hauna mpira penda sana kukaba kupitia viungo na sio mabeki, hii itasaidia hizo though balls kufika kwa walengwa.

Humo ndani kuna timu inaitwa Classic Eleven, kuna wakina Pele, Zico, Kouman, Eric Cantona n.k naomba nisiongee chochote juu ya hii timu ila kiufupi hamna timu ndani ya FIFA 14 kuifunga timu hii.
 
FIFA ni nzuri naipenda because ni ngumu na ina challenge tofauti na PES ni nyepesi sana japo ina ligi nzuri,

kwa beginners wa games ukizoea PES basi FIFA hutaiweza.

all in all nacheza zote kulingana na mood.
Unajua nini Mkuu, hata mimi katika Games niliizoea PES ila baadae nilivyoingia katika Fifa niliiona ngumu, unajua ni nini nilichokifanya? Nikaanza kuweka level ya Beginer, baadae Ameture na baadae professional, hapo kwenye professionar ndo mpaka sasa, yaani kwenye League nacheza level hiyo tu.

Baada ya hapo nikaanza kuipenda FIFA na mpaka sasa nacheza FIFA tu, nacheza PES kama hakuna FIFA.
 
Hawa beginners ndio wanaishabikia PES zaidi kuliko FIFA, FIFA ni mnyama mwingine bhana.
Ndio Mkuu FIFA lazima UWE PRO
najua karibu wote tulianzi pes kule kwenye ps2 ndo maana watu naishabikia. wajaribu FIFA waone mziki
 
Mimi Fifa nishawahi kuwaburuzaga watu sana pale DIT ila baadae nilivyopoteza PC sikucheza kama miezi 4 au 5, nilivyoenda nilifungwa kila mechi.
 
Processor ipoje?
 
PES hawana ishu kabisa aisee,eti mchezaji anaweza kufunga katikati ya uwanja kizembezembe tu yaani...nenda FIFA km utascore magoli kizembe hivyo
 
PES ALL DAY!!, Japo still sometimes nacheza sana FIFA but na ENJOY sana napocheza PES than FIFA,



Kwenye PES mambo sijui ya kuongeza power ya shoot sijui kufunga katikati ya uwanja haya mambo hakuna huku thus why watu wanaocheza sana FIFA akija kwenye PES ilitamsumbua kidogo tofauti na PES player akicheza FIFA.



Yeah, but am still big fan of PES!

 
Sorry chief out of topic, nikicheza gem ya mpira mwili wangu hauna tatizo, ila nikicheza gem za mishen kama GTA, Uncharted na mengineo iwe kwenye console au pc lazma nihisi kizunguzungu, hapo tatizo linaweza kuwa nini? japo kuna jamaa yangu amenambia nitafute miwani kwa ajili ya kichwa.
 
Chief-Mkwawa,
Hiyo unacheza ni ya PC ama PS? Kama PC, aise nisaidie link ya kupata huo mzigo, pes 2018 na patch yake.
 
Ukitaka pes iliyokamilika na timu zote zina jezi viwanja vyote n kutafuta ambazo zimekuwa reparked na zna angalau GB 7 kam ni chini ya GB hizi tegemea kupata setup ambayo viwanja ni vitatu tu, timu za epl zote majina sio halisi wala jezi hakuna.

Me nina pes yangu 17 ni tamu sana jezi zipo zote, viwanja kama 45 hivi mipil ndo usiseme mingi sana, kwa kila timu kuna jezi 3.
Na hakuna haja ya kuwa na patch, iko poa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…