Gamondi Gamondi Gamondi nakuita mara tatu

Kuna kampeni ya chini chini imeanzishwa Gamondi aonekane mbaya, inatoka FC [emoji2772] na kuna watu wanaingizwa king
 


Midomo tu.
Si muende mpeleke CV mpewe Timu mfundishe.


[emoji736][emoji736] you are absolutely right

Leo mmeamua kuiita kampeni za wasioipenda Yanga na kujitoa kwenye sehemu ya wanao laumu mwenendo wa kocha.

Lakini nani asiyejua emotions za mashabiki wa Bongo kwenye timu zao za ndani?

Siku zote timu inapopata matokeo ndio kipindi ambacho unaweza kushuhudia mshikamano wa mashabiki katika kutoa maoni ya timu.

Lakini timu ikipoteza. Hayo yote mliyosema yanasemwa na wasioitakia mema Yanga mtayasema nyinyi.

Kati yenu hapo wapo waliotoa lawama kwa Kocha kwenye mechi ya juzi na sababu zilizotolewa zilikuwa ni hizi hizi ambazo wengine wakizitoa wanaonekana mamluki.
 
Kama kuna mtu ana laumu eti Yanga inashindwa kufanya vizuri mechi za klabu bingwa sababu ya kocha hafanyi rotation basi huyo hajui mpira na hajui rotation hufanywa wakati upi au kipindi kipi. Ningeona wanaakili na wanajua mpira endapo hizi kelele za rotation ningezisikia baada ya kutolewa kikosi cha Yanga vs Mtibwa tarehe 16. Hiyo ndio mechi inayohitaji wachezaji kuwafanyia rotation.

Mtu anakwambia kocha hana mbinu bora ya Nabi, Nabi mbinu zake anazitengeneza kwa kumlenga mshambuliaji mahiri anayewania tuzo kwasasa. Mayele hakukosa mechi hata moja ya kombe la shirikisho na ndiye aliyechochea mafanikio ya Yanga. Ila leo mtu anatoa mlinganyo na mtu anayetumia Musonda na Mzize kama washambuliaji tegemeo. Huyo Nambi kwa mbinu zake mbona kashindwa kuibeba Far Rabat kucheza makundi?
 
Gamondi ni miongoni mwa wale makocha wanao amini the wining team never change...

Hii ubaya wake ni yule anayekaa benchi kila mechi kiwango chake kinadorora tofauti na yule anayecheza kila mechi ambaye kiwango chake huongezeka maradufu...

Tuombe majeruhi yatupitie mbali tusije tukapoteana.
 
We fala ndio hujui mpira, sie tunaongelea comparison ya squad rotation kati ya Nabi na Gamond then wewe unaleta uharo kunuka hapa.
Msimu uliopita wachezaji karibia wote walikuwa wanacheza tena kwa viwango vya juu Sureboy aliupiga mwingi kwa waarab mpaka wakashangaa, moloko, farid mussa na nkane mpaka ngushi wote walicheza kwa zamu na walikuwa wanakiwasha, ilifika wakati yeyote akianza ni sawa na aliye benchi kocha kazi yake ikawa kuangalia match hii nani anaendana nayo anamuingiza na ndio maana timu ikawa kipindi cha pili inabadilika. Lakini huyu Gamond hana hilo yeye mbinu yake ni kuwatumia wachezaji haohao wakifeli siku hiyo ujue mmekwisha, sisi wengine sio mashabiki maandazi kama nyie kila kitu mnaunga mkono.
 
Watacheza tu una haraka gani?
 
Mimi ni mwananchi Kwa hili naungana na wewe
 
Jibu hoja yake inamashiko sana mbona wakati wa Nabi walipata nafasi kwanini sasa?
 
Unataka kocha aweke ghafla tu new faces kwenye mechi ngumu za klabu bingwa Unaujua mpira kweli wewe?
Wewe ndo akili huna, Nabi kafanya rotation mechi za nusu fainali hadi fainali na team imecheza vizuri, sembuse mechi za group stage. Me nikwambie kitu, hawa kina pacome wataanza kupata injury muda sio mrefu, fatigue ipo juu sana kwao, washageuka kauka nikuvae.
 
Walikuwa wanacheza dhidi ya mechi ngumu za kimataifa dhidi ya Club Africain, Tp Mazembe na wanafunga
 
Nabi hakuwa na Pacome au Nzengeli
 
Ambaye hamjui mpira ni nyie mnaongea upumbavu na ujinga. Nabi alikaa na Yanga kwa misimu mingapi? Kitendo cha kocha kukaa muda mrefu kinamfanya ajue kila mchezaji ubora wake na madhaifu yake. Wewe unataka kocha aingie hata mwaka hajamaliza ajaribishe kila mchezaji wakati jambo lilishamuadhibu dhidi ya Ihefu.
Halafu malalamiko yamekuwa mengi utafikiri kwenye ligi Yanga imecheza michezo mingi ndio kwanza imecheza michezo 9 tu hapo kuna michezo kibao ya ligi kuu bado game 21 na hapo bado mechi za Azam federation kwanini mnaharaka ya kumpangia kocha?

Yanga kacheza mechi ngumu back to back nne kwenye ligi kuu, hakuha kocha anayehitaji point atacheza kamari ya kumueka nje Aucho ili Sureboy acheze.

Unasema kipindi cha Nabi hadi Ngushi alikiwasha, embu niorodheshee mechi alizochesha Ngushi wakati wa Nabi ni zipi wewe ni wakufata mkumbo usiyejua mpira. Huyo Ngushi kaonekana chini ya Gamond mpaka watu wakamsifia kwenye mechi ya Yanga vs Kaizer chief kuwa alinyimwa nafasi bure chini ya Nabi ila anakitu. Gamond akampanga tena kwenye mechi za ngao ya jamii akageuka mchezaji mwenye kifafa. Haya niambie ni mechi zipi uliona Nabi akimpanga huyo Ngushi?
 
Hata Nabi alipigiwa kampeni kama hii mwanzoni, ili atolewe. Kwa hiyo hakuna jipya hapa.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana hizi chokochoko zinaanzishwa na wachezaji wanaokosa namba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…