Gamondi hana maisha Yanga

Gamondi hana maisha Yanga

canfi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,368
Reaction score
1,477
Huku game dhidi ya Mashujaa ikiwa ngumu, amewatoa Aucho na Pacome waliokuwa wanaichezesha vyema timu. Baada ya hapo game ikawa ngumu sana na timu pinzani wakaanza kuja bila woga.

Nadhani hajajua kuiheshimu ligi hii. Ikumbukwe kuwa alibadili sehemu kubwa ya kikosi dhidi ya Ihefu, kilichotokea kinafahamika.

Ameshindwa kabisa kuweka uwiano sawa kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na wale wa akiba. Siku zake zinahesabika
 
Sio kweli wachezaji sio maroboti ukiangalia Pacome alishachoka, wachezaji wametumika sana angalia yanga amecheza gemu back to back fatique na aliwatoa kwa ajili ya gemu ngumu ya prison kumbuka yanga kesho yupo safarini tarehe 10 warm up tarehe 11 anacheza, ratiba ngumu sana hii kwa yanga.
 
Bado hamjasema "....yani mpaka mseme......" 😁😁😁
Na mtasemaaaaa 😀😀😀
 
Sio kweli wachezaji sio maroboti ukiangalia Pacome alishachoka, wachezaji wametumika sana angalia yanga amecheza gemu back to back fatique na aliwatoa kwa ajili ya gemu ngumu ya prison kumbuka yanga kesho yupo safarini tarehe 10 warm up tarehe 11 anacheza, ratiba ngumu sana hii kwa yanga.
uliangalia game? au ulihadithiwa, unabisha vitu vipo wazi kabisa.
 
Sio kweli wachezaji sio maroboti ukiangalia Pacome alishachoka, wachezaji wametumika sana angalia yanga amecheza gemu back to back fatique na aliwatoa kwa ajili ya gemu ngumu ya prison kumbuka yanga kesho yupo safarini tarehe 10 warm up tarehe 11 anacheza, ratiba ngumu sana hii kwa yanga.
Kazi ya wachezaji ni nini?
 
Wewe nawe wachezaji wametumika wapi wakati walipewa bata zaidi ya mwezi. Huwezi kufikiria ya kesho kabla ya kuwa na uhakika wa asilimia 100 na ya leo.

Kocha alichofanya leo ni kosa kubwa sana katika mechi ngumu. Unaanza kwanza kuhakikisha unapata alama tatu za leo kisha ndio ujiandae kwa yajayo
 
Huku game dhidi ya Mashujaa ikiwa ngumu, amewatoa Aucho na Pakome waliokuwa wanaichezesha vyema timu. Baada ya hapo game ikawa ngumu sana na timu pinzani wakaanza kuja bila woga. Nadhani hajajua kuiheshimu ligi hii. Ikumbukwe kuwa alibadili sehemu kubwa ya kikosi dhidi ya Ihefu, kilichotokea kinafahamika.

Ameshindwa kabisa kuweka uwiano sawa kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na wale wa akiba. Siku zake zinahesabika
nakubali hana maisha marefu atafukuzwa soon
 
Sawa tunashinda ila Gamondi bado sijamuelewa
Kwa mechi ya Kagera na mechi ya leo amenistajabisha maamuzi yake. Kwa mechi ya Dodoma jiji ni wachezaji ndio walikuwa changamoto katika utulivu. Mapumziko waliyotoa kwa wachezaji wa Yanga yataleta athari kubwa sana kwa Yanga
 
Wewe nawe wachezaji wametumika wapi wakati walipewa bata zaidi ya mwezi. Huwezi kufikiria ya kesho kabla ya kuwa na uhakika wa asilimia 100 na ya leo.
Kocha alichofanya leo ni kosa kubwa sana katika mechi ngumu. Unaanza kwanza kuhakikisha unapata alama tatu za leo kisha ndio ujiandae kwa yajayo
Upo sahihi kocha alicheza kamari kubwa Leo.

Pengo la Diarra limeonekana Leo .Yule dogo msheri hamna kitu huenda Hata metacha asingefungwa lile goli .

Halafu Huyu Joseph guede amesajiliwa kwa pendekezo la kocha au ali kamwe na privaldinho?

Haiwezekani mchezaji yupo uwanja haonyeshi juhudi yoyote halafu akitolewa anacheka.

Waliomleta walitumia vigezo gani kumleta?

Hili ni kosa kubwa sana la kiufundi hasa kwa jinsi kina kamwe na mwenzake walivyompigia debe vya kutosha .
 
Upo sahihi kocha alicheza kamari kubwa Leo.

Pengo la Diarra limeonekana Leo .Yule dogo msheri hamna kitu huenda Hata metacha asingefungwa lile goli...
Guede wamemjaza maneno ya ukubwa. Nina wasiwasi Ali Kamwe na Priva wamemjaza sifa na kuonekana kama yeye ndiye kabebeshwa mzigo wa muarobaini wa tatizo la ubutu wa forward Yanga. Kwahiyo anacheza huku akili yake ikikosa utulivu
 
Ila kusema ule ukweli; kocha anatakiwa abadilishe mfumo wa uchezaji wa timu.

Nahisi huu mfumo wake wa sasa umezoeleka, na pia ni rahisi kwa timu pinzani kuudhibiti kwa njia nyepesi tu ya kupaki basi.
Kagera sugar walifanikiwa, na hivyo kupata sare! Na Tabora United + Mashujaa, na wenyewe wametumia njia ile ile! Mwisho wa siku Yanga wameshinda mechi zote mbili kwa mbinde kweli kweli.

Tukija kwenye mechi ya leo, ni kweli kocha alichemka kumtoa Aucho na Pacome. Wachezaji waliostahili kutolewa mapema walikuwa ni Mzize na yule Guede wake ambaye kwa dakika zaidi ya 80 alizocheza; kwa kweli hakuna alichokifanya ndani ya uwanja.
 
Binafsi sub akitakiwa atoke fred, kibabage, guede na mzize.

Kocha hana shinda, hata NABI kuna game nyingi tu tulishinda 1:0 au 2;1 na droo zilikuwepo pia, so kocha hana shida, shida ni sisi mashabiki kutaka gamond afanye tunachotaka sisi, hii sio professional
Lkn kwa ubora zaidi kocha afundishe forward na winger wajue kuforce na kuwakabili mabeki pinzani.
Muda bado upo
Gamond sio tatizo.

Binafsi kocha tutamdai ubingwa.
Mara nyingi na kwa timu nyingi duniani hutokea timu kushuka kiwango na ligi ikiwa inaendelea

MUHIMU UBINGWA NA TUNA 60% za ubingwa.
Kocha hana baya wala wachezaji.
Okra ni ingizo muhimu sana, atatufaa
Yule fred atupishe.
 
Kwa mechi ya Kagera na mechi ya leo amenistajabisha maamuzi yake. Kwa mechi ya Dodoma jiji ni wachezaji ndio walikuwa changamoto katika utulivu. Mapumziko waliyotoa kwa wachezaji wa Yanga yataleta athari kubwa sana kwa Yanga
Mi naona Yanga walianza game kwa pressure kubwa walitaka wamaliźe game mapema,ile game ilihitaji utulivu kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli wachezaji sio maroboti ukiangalia Pacome alishachoka, wachezaji wametumika sana angalia yanga amecheza gemu back to back fatique na aliwatoa kwa ajili ya gemu ngumu ya prison kumbuka yanga kesho yupo safarini tarehe 10 warm up tarehe 11 anacheza, ratiba ngumu sana hii kwa yanga.
Sasa unawapumzishaje manguli wa timu wakati huna uhakika wa ushindi?
 
Back
Top Bottom