Toka Mamelodi ilipotangazwa kucheza na Yanga, uongozi wa Yanga ulishaanza kujenga mazingira ya jinsi ya kujitetea na zahma iliyo mbele yao. Mapema sana viongozi na mashabiki walishaanza kuchanganyikiwa.
Walitaka wachezaji wao wasiitwe timu ya taifa wakati huo huo wakalalamika saaana kwa nini Dickson Job hajaitwa, hiyo ni dalili ya watu waliochanganyikiwa. Wakaja kwenye majeruhi ya Pacome mara ishu ikabuma kwa kuitwa na kwenda timu ya taifa, eti anaenda kuangaliwa na madaktari wa timu ya taifa, dalili nyingine ya watu waliochanganyikiwa. Wakaja kwenye vitisho vizito dhidi ya watakaovaa jezi za Mamelodi, baada ya kelele nyingi na barua nzito kutoka CAF, wakanywea.
Sasa hivi wanasema kina Diarra hawajarudi mpaka sasa na wale ambao walisema wameshapona wanadai wanaweza kuwakosa. Dalili za watu waliochanganyikiwa. Hizi taarifa ndiyo kabisa zitafanya mashabiki wao hata wale wa bure wasije uwanjani.
Hii mechi Yanga ingekaza bila kucheza hizi mind games ingeweza kutoboa. Tatizo imefanya mambo yamekuwa mengi.