Gari inashtuka nikikanyaga mafuta baada ya kusimama

coyyote

Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
53
Reaction score
88
Habari wakuu, nna gari aina ya Toyota Ractis model ya 2006, tatizo lake ni kwamba kila nikisimama alafu nikakanyaga mafuta gari inashtuka kwanza alaf ndio itatembea, nimeshaenda kwa mafundi wawili lakini sijapata jibu la tatizo langu.

Kama kuna mtu mwenye uzoefu ama utaalamu wa tatizo kama ilo naomba msaada tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kacheki Sensor ya pump ya mafuta iliopo mbele kwenye bonet..
 
Hata mimi huwa inanitokea, ila nilichogundua ni kwamba mfano ukiwa umesimama ukawasha gari hapohapo ukakanyaga mafuta lazima istuke kidogo ila mfano ukiiwasha ukasubiri kama sekunde tano ukikanyaga mafuta haistuki
Na mara nyingi ukiizima kwenye foleni then ukaiwasha na kuondoka ghafla ndo inastuka ila kama upo sehemu ukaizima kabisa ukafanya mambo yako hata ukiiwasha na kukanyaga mafuta huwa haistuki. Kwa hiyo nilichojifunza kwenye gari yangu ni kuwasha then naisubiri km 5 to 10 second then nakanyaga mafuta, kwa kufanya hivo gari haistuki
 
Mimi bila ata ya kuzima, ata nikisimama kwenye foleni af nikaanza kutembea inashtuka, mafundi waliniambia labda tubadili oil ya gearbox lakini tatizo bado halijaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi ni kwanini watu wanapenda kuzima gari wakiwa kwenye foleni....nashindwa kuelewa huwa wanafikiria nini!!!
 
hivi ni kwanini watu wanapenda kuzima gari wakiwa kwenye foleni....nashindwa kuelewa huwa wanafikiria nini!!!
Brother mafuta yanatembea kwenye foleni kwa hiyo watu wanaopt kuzima, kama upo nje ya Dar mtu akikuambia foleni inavotesa huwezimwelewa. Kuna kipindi unaweza ukakutana na foleni ya kufa mtu ama msafara wa mheshimiwa aisee huweziliacha gari linaunguruma lazima ulizime usikilizie kwanza mpaka foleni ianze kutembea
 
Mimi bila ata ya kuzima, ata nikisimama kwenye foleni af nikaanza kutembea inashtuka, mafundi waliniambia labda tubadili oil ya gearbox lakini tatizo bado halijaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kutakuwa na tatizo aisee, cheki na fundi wa uhakika si kila fundi wa magari ana utalaamu wa kila part ya gari, endelea kufanya research taratibu utakutana na fundi wa kukusaidia kutatua tatizo hilo kama upo Dar nenda pale maeneo ya Sinza kijiweni baada ya kituo cha mafuta cha Puma kuna gereji wale jamaa huwa wanajitaidi
 
Hilo ni tatizo la wanaume wa dar
Hahahaha mikoani hamwezijua hii kitu kinachoitwa foleni ambapo unakaa zaidi ya saa sehemu moja kusubiri foleni itembee ama kumsubiri mheshimiwa apite kwa hiyo ruksa kutuita wanaume wa Dar
 
Kwamaelezo hapo juu ya wadau wawili tofauti yawezekana shida ipo kwenye gearbox.kwanza hiyo gari nahisi inatumia CVT gearbox je huwa unaweka hydrolic ya aina gani??.

Kwa maelezo yenu shida ipo hivi inaonekana kama kuna sehem kwenye gearbox kupo loose kama sio clutch basi kuna diaphram au seal zitakuwa zimekauka so zinasababisha kuloose pressure au waweza sema chujio limechafuka..

So unapoweka gear kuna kuwa na utofauti kati ya mzunguko wa engine na gearbox..yaani ni sawa na gari ya manually ukaweka gear harafu ukakanyaga clutch ukaweka number 1 badala ya kuachia clutch mdogo mdogo ww ukaachia full kwa mara moja lazima gari itastuka..ndio kinachotokea hapo.au kama gari diffu ikiwa bovo au ikiwa na play lazima ukiweka gia inastuka..natamani ningeiona hiyo gari ningekwambia shida ni nn??.au kama unaweza piga jeki harafu angalia kama kuna play kwenye vikombe vya kwenye gearbox..piga jeki weka p harafu chezesha tairi mbleye nyuma uone kama ina play
 
Yes ni ina cvt gearbox mkuu maana kuna button Ipo pembeni ya gear imeandikwa cvt sport, wapi naweza pata mtaalamu wa hili tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hapo awali ulikuwa unatumia gearbox oil ya aina gani
 
Yes ni ina cvt gearbox mkuu maana kuna button Ipo pembeni ya gear imeandikwa cvt sport, wapi naweza pata mtaalamu wa hili tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Historia ya hiyo gearbox kuanza kufanya hivyo?? Ni baada ya kufanya matengenezo flani?? Kama kubadili hydrolic ya gearbox au ilianzaje anzaje??. Mara nyingi wengi huwa wanaweka hydrolic za kawaida so shida kama hizo ndio huanzia hapo
 
Historia ya hiyo gearbox kuanza kufanya hivyo?? Ni baada ya kufanya matengenezo flani?? Kama kubadili hydrolic ya gearbox au ilianzaje anzaje??. Mara nyingi wengi huwa wanaweka hydrolic za kawaida so shida kama hizo ndio huanzia hapo
Yaaani gari nimetoka kuichukua yard nikakutana na ichi kitu, ina kama miezi miwili kwaio sijagusa chochote zaidi ya kuifanyia service ya kawaida tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafundi watakuharibia gari sio kila unayemkuta gereji ni Fundi hilo tatizo linaweza kuwa ni tatizo dogo sijui kufungua gear box unaweza kuzalisha tatizo jingine, sasa nikuulize umewahi kuosha Engine? Kama jibu ni ndio kuna baadhi hawajui kuosha Engine za magari hasa gari ya Petrol inahitaji umakini sio kila mtu anajua kuosha Engine,maji mara nyingi maji yakiingia kwenye plug yanaleta hilo tatizo peleka kwa Fundi aangalie plug zote kama ziko sawasawa,maana kama plug zinashindwa kuchoma mafuta sawasawa gari huwa inashtuka
 
Mkuu, kwanza naomba nikupongeze kwa kumiliki mkebe in town....
Pili sina la kukushauri, ebu tusubiri wanaojua hizo mambo wakuje
 
Kweli kabisa mm gari ilikuwa haipati nguvu Mara tukabadili pump Mara nikaambiwa plugs mwisho nikaamu kwenda kuipima majibu yakatoka tatizo ni air sensor nikabadili hadi Leo tatizo limeisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…