Car4Sale Gari inauzwa Mitsubishi Pajero (2004)

Kwenye browser zinaonekana, sijawahi kupata hilo tatizo
Yeah its true. Shida watu wengi hawatumii browser wanatumia app. Sasa JF wamekaa kimya hawatatui tatizo la app kutoonyesha picha Maxemello sijui kawaje yaani na yeye.
 
10m hailipi tajiri??
Dah huko ni chini sana ya budget boss wangu ongezea hiyo tano hapa tufanye biashara. Gari ni nzuri hii. Haina shida. Mafuta inatumia vizuri kwa wanaozifahamu SUV's, ipo kwenye uimara wake. Mtumiaji ni mkurugenzi wa kampuni na hakuna mtu alishaimiliki toka ilipokuja tokea Japan.

So ipo vema. Njoo uikague gari nipe mawasiliano yako hapa DM tumalize biashara. Hii kama utaichukua utaweza hata ifanyia decorations then ukaja pata mteja wa bei ya soko ni vile tu kwasasa nipo chini ya maagizo ya kuiuza haraka ndio maana nauza bei hiyo, hiyari yangu hii isingeuzwa chini ya milioni 24.
 
Imebidi nikujibu tena maana nimeona nikikuacha na huu ujinga unaweza kwenda kuaibika ukweni au ukashindwa kununua gari nzuri sababu tu hauna elimu juu ya matumizi yake.

Hizi gari zinakuja na mfumo wa kubadili matumizi ya nguvu za tairi.

Kwa mfano hii, unaweza tumia tairi zote 4 yaani ziwe zinasukuma na kuvuta gari,yaani 4WD au unaweza tumia tairi za nyuma tu kusukuma gari yaani 2WD.

Hii function sio automatic ni manually engaged. Mfano ukiwa mjini hapa huna haja ya kuweka 4WD function bali utatumia 2WD na ndipo hapo utaona kiwango cha matumizi ya mafuta kikishuka sana inaweza kukupa hata 1litre = 13.5 hadi 14km kama hautakuwa unatumia AC muda wote, na hata hivyo itategemea AC umeweka katika mode gani kama umeweka low mode ina maana AC haitohitaji kuvuta sana nguvu ya gari kurun so itakupa good consumption ya mafuta.


So hivi ndivyo namna hii gari inaweza kuwa economy kwenye mafuta na ukiwa upo safari nje huko ya mji ukipanda vilima na kushuka makorongo au barabara za tope ndipo utaona uzuri wa hii gari sababu utaweka full function ya 4WD na utaona ikiwa na power ya kukutoa barabara ya mchanga, tope au maji kwa irahisi bila shida.

Kuna mataifa kama Indonesia wanazitumia sana hizi gari kushinda Toyota na zinawapa matokeo mazuri. Uoga wa brands ulikuwa sahihi miaka ya nyuma ila sio sasa ambapo kuna unafuu wa spare, ni rahisi kupata spare na elimu sahihi juu ya matumizi na matunzo ya magari ipo hewani.

Hizi gari (Pajero Mitsubishi) ni miongoni mwa gari ngumu na vumilivu kwa mazingira yetu. Ni vema kufahamu kitu kwa undani na sio story za kuambiwa.

Mimi nimelitumia ndio maana nazungumzia hivyo.
 
Huwa napenda kutolewa ujinga Yes... kwahiyo kinachofanya ulaji wa mafua kuongezeka ni ukubwa wa Engine au 4WD?
 
Huwa napenda kutolewa ujinga Yes... kwahiyo kinachofanya ulaji wa mafua kuongezeka ni ukubwa wa Engine au 4WD?
Kuna combination ya Factor kwann gari inywe mafuta mengi, nitakupa list ya sababu.

1. Air cleaner ikiwa chafu mafuta yataenda.
2. Spark plugs zikiwa hazifanyi kazi vizuri itaathiri eneo la mafuta.

3. Tairi zikiwa hazina upepo vizuri, mafuta yatalika.

4. Uendeshaji wako kama dereva ukiwa mtu wa kukanyaga accelerator pedal kwa nguvu sana tegemea mafuta kulika.

5. Kuweka oil ambayo sio sahihi inafanya mafuta kulika.

6. Nozzles zikiwa zimekaa vibaya kuna uwezekano zikatema mafuta mengi sana so mafuta yakalika.

Sababu ni nyingi sana huwezi tazama tu CC za gari kama kisababishi cha mafuta kulika kwa kasi.

4WD inakula mafuta ila kwa standard ya matumizi sio ile inakula kwa upotevu, No.

Jambo lingine unatakiwa kufahamu ni kuwa gari inaweza kuwa na Cc 4,500 ila ikawa inakwenda km nyingi kwa lita moja ya mafuta kushinda hata IST. Hii inatokana na technology inayotumika ngoja nikutumie kiambatanishi cha mfano hapo chini.
 
3500CC na 1200CC engine technically ipi inatumia mafuta mengi?
 
Huwa napenda kutolewa ujinga Yes... kwahiyo kinachofanya ulaji wa mafua kuongezeka ni ukubwa wa Engine au 4WD?
Tazama mfano hizi gari mbili. Alphard hybrid ambayo ni cc karibia 3,000 ila inakwenda lita 1 kwa Km 26 .

Harrier hybrid inakula 1 kwenda km 21.

So unaweza imagine kuwa CC sio tu Factor kubwa ya kutazama hapa.
 
Hiyo Pajero ni hybrid?
Sio hybrid, hybrid, zipo. Ila hii Pajero ni miongoni mwa gari zilitengezwa kwa kutazama factor ya fuel efficiency ndio maana wakaweka option ya kuchagua gari itembelee 4WD au 2WD.

Kuna gari hazina hiyo option na mafuta zinatumia sana tu. Sababu zipo locked on 4WD hakuna option ya kuchange hapo.
 
3500CC na 1200CC engine technically ipi inatumia mafuta mengi?
Kama nilivyosema awali ukitumia CC kidefine unywaji wa mafuta wa gari utakosea sana. Cc kubwa gari huwa inakula mafuta ila sasa itategemea.

Kuna gari CC ni 4,500 huko ila mafuta inatumia kidogo sana sababu zinakuwa na mota inayosaidia kurun engine so mafuta yanakwenda kidogo sana.

While kuna gari ni CC 2,500 tu ila inakula mafuta kama meli. Unaifahamu Nissan Fuga, Hammer, brevis etc.


Sasa kuna mtu ukimtajia Alphard au Harrier hatakuelewa ukimwambia inatembea km 26 kwa lita moja. Kitu ambacho hata passo au IST haifanyi so ni elimu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…