Kuna combination ya Factor kwann gari inywe mafuta mengi, nitakupa list ya sababu.
1. Air cleaner ikiwa chafu mafuta yataenda.
2. Spark plugs zikiwa hazifanyi kazi vizuri itaathiri eneo la mafuta.
3. Tairi zikiwa hazina upepo vizuri, mafuta yatalika.
4. Uendeshaji wako kama dereva ukiwa mtu wa kukanyaga accelerator pedal kwa nguvu sana tegemea mafuta kulika.
5. Kuweka oil ambayo sio sahihi inafanya mafuta kulika.
6. Nozzles zikiwa zimekaa vibaya kuna uwezekano zikatema mafuta mengi sana so mafuta yakalika.
Sababu ni nyingi sana huwezi tazama tu CC za gari kama kisababishi cha mafuta kulika kwa kasi.
4WD inakula mafuta ila kwa standard ya matumizi sio ile inakula kwa upotevu, No.
Jambo lingine unatakiwa kufahamu ni kuwa gari inaweza kuwa na Cc 4,500 ila ikawa inakwenda km nyingi kwa lita moja ya mafuta kushinda hata IST. Hii inatokana na technology inayotumika ngoja nikutumie kiambatanishi cha mfano hapo chini.