kumbe jibu unaalo kuwa gari nyenye CC ndogo ndo haitumii mafuta mengi? anyway! Gari yoyote ya CC kuanzia mia 900-1300 ni bora zaidi. mkuranga si mbali kwa gari yeyote kufika kwani ni mkeka mwanzo mwisho.
Mimi natumia Hyundai i10 kama za Voda zile mafuta ya Elfu kumi unaenda TEGETA mwisho na kurudi Tokea SEGEREA, mkuranga inakanyaga sana tu, waweza nunua hizo pale Hyundai, Nyerere Road, ziko fiti.
Nunua RAV 4
wenye uzoefu na magari nisaidieni, nahitaji kununua gari
my concern;
1. iwe na consumption ya mafuta kiasi...
2. mahali ninapoishi na ofisini ni km 20 kwenda 20 kurudi kila siku
3.most wkends nina misele ya mkuranga na mlandizi (nina vijibustani huko lol)
4. nafikiria kununua cami au swift je zitamudu hayo masafa? na je hazisumbui?
5. nilikuwa na gari yenye cc 2200 ila hiyo hela ninayopoteza kwenye mafuta naona ni bora niingize kwenye vijiproject vyangu huko mkuranga,nahitaji gari itakoyonimuvuzisha from point A to B full stop.
6. na-prefer gari isiyozidi cc 1300.
Ushauri tafadhali.
hatimaye ng'ombe wamerudi zizini..!!! mtu angeambiwa akachonge tairi za kimasai
Mi nishasahaugi siku nyingi kuangalia gari based on fuel consumtion! Mi naona yote sawa tu. Bora ufike unapotaka
kama unaweza ku-afford mafuta ya mawazo - why to buy a car? get one stroke ki-Bajaji -- the point is to move from point A to B: as i do.
rav 4 nyingi zinaanzia cc 2000, nahitaji gari isyozidi cc 1300
Cami ndio "mwake"
1) Iko juu so vibonde uchwara inapeta tu.
2) CC ndogo so ni economical kwenye mafuta.
3) 4WD so matope na vijimlima mshenzi havikusumbui.
4) Ni Toyota ambapo spare bwerere.
5)Kwa we mdada itakutoa kidogo, manake nacho kana sura nzuri tu.
Ila sasa Cami ana pacha wake anaitwa Daihatsu Terios, huyu sina uhakika sana nae kama wanafanana kila kitu na Cami pamoja na kuvaliana spares.
Kweli kaka/dada if you cannot afford to maintain a car why not buy a bicycle. Hivi unajua Waziri kama Vince Cable (waziri wa biashara na Viwanda UK) anaendesha baiskeli kwenda ofisini kwake. Meya wa London Boris Johnson naye pia anaendesha baiskeli kwenda ofisini kwake. Na ukiwaona wana afya nzuri sana. Sisi tuna masukari, mablood pressure, vitambi kwasababu hatuna exercise yeyote. Gari yeyote utakayonunua itakuwa ina manufaa na hasara zake. Unaweza kununua Hyundai i10 but ukawa usalama wako uko hatarini, barabara nyingi huwezi kupita, safari ndefu hazifiki zinachemsha n.k. Vile vile unaweza kununua V8 ukawa unatumia mafuta mengi bila ya sababu (mfano kuendesha katikati ya mji kama Dar), parking tabu nk.