Gari ipi itanisaidia kubana matumizi

Gari ipi itanisaidia kubana matumizi

kumbe jibu unaalo kuwa gari nyenye CC ndogo ndo haitumii mafuta mengi? anyway! Gari yoyote ya CC kuanzia mia 900-1300 ni bora zaidi. mkuranga si mbali kwa gari yeyote kufika kwani ni mkeka mwanzo mwisho.

Mimi natumia Hyundai i10 kama za Voda zile mafuta ya Elfu kumi unaenda TEGETA mwisho na kurudi Tokea SEGEREA, mkuranga inakanyaga sana tu, waweza nunua hizo pale Hyundai, Nyerere Road, ziko fiti.


senkyu mkuu nafanyia kazi ushauri
 
wenye uzoefu na magari nisaidieni, nahitaji kununua gari

my concern;
1. iwe na consumption ya mafuta kiasi...
2. mahali ninapoishi na ofisini ni km 20 kwenda 20 kurudi kila siku
3.most wkends nina misele ya mkuranga na mlandizi (nina vijibustani huko lol)
4. nafikiria kununua cami au swift je zitamudu hayo masafa? na je hazisumbui?
5. nilikuwa na gari yenye cc 2200 ila hiyo hela ninayopoteza kwenye mafuta naona ni bora niingize kwenye vijiproject vyangu huko mkuranga,nahitaji gari itakoyonimuvuzisha from point A to B full stop.
6. na-prefer gari isiyozidi cc 1300.

Ushauri tafadhali.

Kamata VW mgongo wa chura utadumu nayo kwa muda mrefu
 
...Tafuta Suzuki Sierra,iko na cc 660 halafu ni 4wd,una engage kama Hardtop!!lita 1 waweza kwenda mpk km 35,lol!!vitz,duet,swift pia s0i mbaya.

ubarikiwe for this info.
 
Sister choose Cami kama bustani zako zinakubidi kuingia barabara mbovu, sababu ipo juu na hakili mafuta,, Wataalamu wa magari mngenisaidia na mimi pia Kuna kigari nimekiona mtandaoni CIF DAR imenivutia kinaitwa Suzuki Aerio kina cc kama 1500 hivi, price yake na shape kamenivutia sana kwa routes zangu za Dar, but wasiwasi upo kwenye spare parts zake zinapatikana dar? au zinaingiliana na Swift,, msaada jamani nataka nikiwahi kabla hakijauzwa kwenye hiyo website
 
Cami naona kama ni nzuri iko juu hata kwa shep inapendeza, vtz imekaa kidada sana hata Mr ataogopa kutoka nayo

duu kumbe nilitakiwa nilimkumbe na mr pia kwenye kuchagua gari senkyuuu
 
hatimaye ng'ombe wamerudi zizini..!!! mtu angeambiwa akachonge tairi za kimasai


Kweli angalau siku hizi watu wamekuwa wastaarabu. Mwenzio anauliza unajibu utumbo.., si utoto huo, tena afadhali utoto huo unakuwa ni u~#^-/x . Tuendelee kuwa wastaarabu namna hiyo ili mtu akifika JF akute waerevu watupu. Wale wapumbavu wachache wanaojibu ujinga wataokoka nao pia.
 
Mi nishasahaugi siku nyingi kuangalia gari based on fuel consumtion! Mi naona yote sawa tu. Bora ufike unapotaka

Nyie mafisadi wa CCM si mnachukua mafuta ya bure kwenye vituo vya kuuzia mafuta kwa kuwasaidia hao jamaa kukwepa kulipa kodi!
 
kama unaweza ku-afford mafuta ya mawazo - why to buy a car? get one stroke ki-Bajaji -- the point is to move from point A to B: as i do.

nahitaji gari ili iweze kunisaidia kufanikisha baadhi ya malengo yangu, ni kweli nina pesa ya mawazo ndio maana nikaomba ushauri kwa hiyo pesa yangu ndogo gari ipi nitaimudu? bajaji sawa lakini bajaji haiwezi kunitoa mbezi ya kawe to mkuranga au mlandizi thanks anyway.
 
Cami ndio "mwake"
1) Iko juu so vibonde uchwara inapeta tu.
2) CC ndogo so ni economical kwenye mafuta.
3) 4WD so matope na vijimlima mshenzi havikusumbui.
4) Ni Toyota ambapo spare bwerere.
5)Kwa we mdada itakutoa kidogo, manake nacho kana sura nzuri tu.
Ila sasa Cami ana pacha wake anaitwa Daihatsu Terios, huyu sina uhakika sana nae kama wanafanana kila kitu na Cami pamoja na kuvaliana spares.
 
rav 4 nyingi zinaanzia cc 2000, nahitaji gari isyozidi cc 1300

Yeah RAV4 4 zinaanzia 2000 cc - 2400 cc na ni full time 4WD kwahiyo zinatafuna zaidi mafuta. Cami ni nzuri ina cc 1300 na ina part time 4WD so itakufaa kwa sehemu korofi.
 
Cami ndio "mwake"
1) Iko juu so vibonde uchwara inapeta tu.
2) CC ndogo so ni economical kwenye mafuta.
3) 4WD so matope na vijimlima mshenzi havikusumbui.
4) Ni Toyota ambapo spare bwerere.
5)Kwa we mdada itakutoa kidogo, manake nacho kana sura nzuri tu.
Ila sasa Cami ana pacha wake anaitwa Daihatsu Terios, huyu sina uhakika sana nae kama wanafanana kila kitu na Cami pamoja na kuvaliana spares.

Hapo kwenye red mkuu siyo kweli. Toyota Cami ni sawa na Daihatsu Terios. Walichofanya ni kuondoa tu nembo ya Daihatsu na kuweka nembo ya Toyota. Kwahiyo spare zake haziingiliani kabisa na Toyota zingine and they are expensive japo ni imara sana ukinunua unasahau.
 
Mtu anafahamu kabisa kuwa consumption ya mafuta ktk gari hutokana na engine cc, hapa huwa sipati tabu kuona kuwa hii ina kuwa kama show off!
 
Kweli kaka/dada if you cannot afford to maintain a car why not buy a bicycle. Hivi unajua Waziri kama Vince Cable (waziri wa biashara na Viwanda UK) anaendesha baiskeli kwenda ofisini kwake. Meya wa London Boris Johnson naye pia anaendesha baiskeli kwenda ofisini kwake. Na ukiwaona wana afya nzuri sana. Sisi tuna masukari, mablood pressure, vitambi kwasababu hatuna exercise yeyote. Gari yeyote utakayonunua itakuwa ina manufaa na hasara zake. Unaweza kununua Hyundai i10 but ukawa usalama wako uko hatarini, barabara nyingi huwezi kupita, safari ndefu hazifiki zinachemsha n.k. Vile vile unaweza kununua V8 ukawa unatumia mafuta mengi bila ya sababu (mfano kuendesha katikati ya mji kama Dar), parking tabu nk.

asante kwa ushauri mkuu, lakini je hali ya hewa ya UK ni sawa na DAR??? leo dar in 28 c wakati Uk yote ni kati ya degree 13-17 C , london ndio wana 20 C , natokea maeneo ya mbezi ya tegeta then unaniambia niendeshe baiskel to nyerere road mahali nafanya kazi? sinitafika nimelowa jasho mwili mzima? au niende na baiskeli mkuranga? ntafika saa ngapi na kurudi saa ngapi? wakati naomba ushauri niliweka pia na concern zangu nadhani ungezingatia mahitaji yangu wakati wakunishauri, vinginevyo sio kila kitu wafanyacho wazungu kinafaa kwa mazingira ya kwetu,
 
Back
Top Bottom