Gari ipi itanisaidia kubana matumizi


Sijasema zinaingiliana na zingine.
Chaser yenyewe haiivi na Mark 2 wala Cresta, sembuse Cami.
Nlichosema ile tu kua Toyota ni advantage kwenye upatikanaji wa spare.
Na ni kweli zinadumu so nafuu,
kwamba waweza kununua spare ya laki 1 ukakaa nayo miaka miwili, ni rahisi kuliko ya Alfu 50 ukae nayo miezi 8.
Otherwise unapokosesha moja, patisha mengine basi nijue nina maksi ngapi.
 
Mtu anafahamu kabisa kuwa consumption ya mafuta ktk gari hutokana na engine cc, hapa huwa sipati tabu kuona kuwa hii ina kuwa kama show off!

unaweza ukaona hivyo ni mtazamo wako sawa, lakini kufahamu consumption ya mafuta peke yake sio kigezo pekee cha kununua gari, kuna vitu kama spear na upatikanaji wake, na uimara wa gari pia, vinginezo naweza kuishia nunua gari ambayo kila mwezi lazima tugawane mshahara na fundi garage, pole kama umekwazika na hili bandiko langu, lakini pia sio kila ukijuacho kipo kama unavyokijua wewe, kuna ambao wanaokijua zaidi yako.
 

shukrani mkuu umenisaidia sana
 

Naam hakuna tofauti yeyote kwa foleni ya dar siku hizi naona bora mtu kuendesha baiskeli kuliko kuendesha V8 katikati ya jiji la Dar.

Umezungumzia distance from Tegeta to Nyerere road maeneo haya yana foleni sana asubuhi na jioni kuanzia mwenge, morocco kwenda tangi bovu. Ushauri wangu unaweza kuendesha baiskeli in between and then kuendelea huko ukachukua gari lako ulilopaki mwenge kwenda zako nyerere road. Wakati wa kurudi kutoka kazini pia unaendesha gari yako mpaka mwenge unalipaki na kuchukua baiskeli au daladala mpaka kwako Tegeta.

Binafsi mwakani mungu akipenda nimeweka malengo nianze kuendesha baiskeli kutokea mahali nakopaki gari yangu hadi ofisini kwangu. Kwani kuanzia mjini (city centre) mpaka ofisini natumia dk 15 kutembea kwa miguu ila kwa gari it takes around 1 hour or 30 minutes. Gari yangu ni CC 2900 na hivyo inamaana kwa safari ya pole pole naweza kuwa natumia si chini ya Tshs 10,000. Bado sijaweka hasara ya gharama za kulika kwa clutch, accelerator, mikwaruzo ya gari nk. Tuseme kama 50,000. Hivyo nitalichukua gari langu hadi karibia na mjini napaki nachukua baiskeli naingia nayo katikati ya mji.

Na wewe jipange ndugu gari yeyote ina faida zake na hasara zake asikudanganye mtu. Nimeendesha gari ya CC 1100 (Suzuki Jimmy), Nimeendesha gari ya CC 2000 , Nimeendesha gari ya CC 1500 na sasa naendesha gari ya CC 2900 sioni tofauti yeyote ni nidhamu ya matumizi tu ndio cha msingi hakuna zaidi.
 
Hebu mwenye data anisaidie nami pia kuna kagari kanaitwa Mazda demio model mpya (sawa na mazda 2 kwa watu wa EU na USA) haka kana CC 1300. Kwa Bongo yetu kanalipa kweli au ndo maumivu kwa kwenda mbele ili kukaweka barabarani?
 

nakushukuru mkuu , barikiwa sana, inshallah naamini ipo siku nitaweza kumudu gari ya cc 3000 lol ila kwa sasa bado nachechemea.
 
nakushukuru mkuu , barikiwa sana, inshallah naamini ipo siku nitaweza kumudu gari ya cc 3000 lol ila kwa sasa bado nachechemea.

Unajua mkuu,

Hujanifahamu unatakiwa kujipanga matumizi yako ya gari na safari unazokwenda. Mfano unaweza kununua gari ya CC ndogo mfano Suzuki Sierra or Jimmy (CC 1100) lakini kutokana na kuamini kuwa una gari ya safari ndogo matumizi ya mafuta yakaongezeka. Matokeo yake ukawa hujasave kitu. Pia gari la CC ndogo lina faida yake na hasara zake. Nimekupa mfano Hyundai i10 hii gari ni nzuri sana ila haijawa design for outside ya mjini (yaani ni city car). Matokeo yake ukiwa na safari ya kwenda labda iringa, Mbeya, Arusha nk kitakuja kukuwakia moto bure. Pia hyundai haina grip (stability kwenye barabara) na kwa barabara zetu bongo lami yenye ya usanii (kwani barabara zetu nyingi zinatengenezwa below standard) matokeo ikinyesha mvua tope la nguvu na magari hayaendi. Zaidi barabara zisizo na lami ndio kabisa kinaweza kukufia huko huko. Wenye Hyundai wanajipa moyo lakini hawawezi kuwa sawa na mtu ambaye ana V8 mfano Toyota Landcruiser. Kwasababu lile limetengenezwa kukabiliana na mazingira hayo.

Mie siamini kubadilisha gari ndio solution ya tatizo lako bali pangilia matumizi yako ya mafuta. Mbona binafsi nikienda kutembelea site zangu huwa napanda mabasi? Wewe unashindwa kitu gani? Au nakwenda jumamosi au jumapili siku ambazo hazina foleni nisitumie mafuta mengi. Na matumizi yangu ya gari hayana tofauti kabisa nikiwa na gari ya CC 2900 au gari ya CC 1500.
 
Binafsi bado natafakari kama Cc za gari zinaendana na matumizi ya mafuta. Tulinunua Daihatsu Terios -KID Cc 690, ni nzuri ina FWD, na A/C tukitegemea tumepiga bao fuel consumption, lakini mahesabu yanaonyesha lita moja ya petrol inatembea Kilometer 9.5 (a/c full time) ambayo ni sawa na Gari ya cc 1500.

Ushauri wangu tafuta Gari yeyote ya cc 1500 ambayo hata ukiamua kwenda safari ndefu unakwenda ila kupunguza matumizi ya mafuta fanya mkakati wa kuplan vizuri mizunguko.
 
nunua Subaru Forester , imekua msaada mkubwa kwangu, mafuta ni economy, spare zipo nyingi mtaani, Imara sana
 
suzuki sierra ni nzuri, Mi mwenyewe nimeshaitumia fuel consumption ni nzuri na pia haihitaji sasa service za mara kwa mara...na pia zina 4WD so hata ukikwama mahali huhangaiki sana.
 

nakushukuru kwa changamoto unazonipatia, ni kweli nahitaji kupangilia matumizi ya mafuta, ndio katika kujiuliza huko nikaona labda nikiwa na gari yenye cc ndogo naweza kuserve cost kidogo.
 
Wazo zuri sana hili la kutumia baiskeli, lakinikwa miundombinu hii ya Bongo, sijui kama linawezekana, usalama wako utakuwa hatarini sana
 
Mkuu wewe ndiye umeongea point mzuri sana kuhusu gari na foleni za Bongo....by theway ushahuri wako wa baiskeli sina budi kuufanyia kazi kutoka leo.....ikiwezekana nitakuwa naipakiza baiskeli yangu kwenye siti za nyuma ya gari langu hadi maeneo fulani,kisha napaki gari,nashusha
baiskeli yangu kisha huyoooo mitaa ya city center....na wakati wa kurejea home ni hivyo hivyo. Kuhusu kuwa na gari yenye cc 1000-1500 ili kubana matumizi ya pesa kwenye mafuta'binafsi huwa siamini kabisa hiyo kitu ndani ya kichwa yangu....Hivi inawezekana vipi mtu ununue gari ya millioni 17 alafu ushindwe kuweka mafuta ya elfu 20-50? Hivyo vigari vya cc 600-1500 ni vigari vya mama wa nyumbani (tene ambaye hana kazi)
pamoja na watoto. Mniwie radhi huu ni mtizamo wangu binafsi!
 
Point.....well said mkuu!
 

mweee JF kiboko...mkuu dongo hilo limetua mahala pake haswa! mwenzio fedha zangu za mafungu sasa hivi napunguza liability naongeza asset mkuu acha tu niwe na hivyo vigari vya wamama wa nyumbani as long as vitatimiza lengo
 
Wazo zuri sana hili la kutumia baiskeli, lakinikwa miundombinu hii ya Bongo, sijui kama linawezekana, usalama wako utakuwa hatarini sana

Kaka usalama ni muhimu lakini kugawana mshahara na gari haina maana. Binafsi naona kama ukiwa na sehemu salama ya kupaki gari yako mfano maeneo ya morocco, mikocheni, oysterbay, bandarini (maeneo ya mivinjeni ), ilala, magomeni ukaweza kuepukana na Triangle of crisis (Upanga, Kariakoo, City centre) maeneo haya unavuta baiskeli na helmet yako unaendesha hadi hapo miundo mbinu ya jiji la Dar itakapoboreshwa. Kulikoni, ukawa unatumia karibia 50,000 kwa saa kwenye foleni bora nichukue baiskeli yangu niendeshe mjini.
 

Kaka/Dada China, Netherlands, UK kuna baiskeli unazikunja na kuwa kama begi la ofisini na nyepesi kama kilo 8-7 ila bei yake achana nayo (yangu nieagizia inauzwa karibia laki nane na upuuzi). Nikifika ofisini naikunja na kuibeba kama begi hadi ofisini. Tatizo linaloniumiza kichwa ni wapi nitapaki gari yangu kwa usalama mpaka nitakoporudi kutoka ofisini. Nilitaka kuweka pale maeneo ya drive-in ila sijafanikiwa ila bado kuna maeneo kama masaki, oysterbay nikipata mahali penye usalama nitapaki gari na kuchukua baiskeli na kuingia nayo mjini. Kusimama kwenye foleni masaa mawili asubuhi na masaa mawili jioni kila siku ni hasara mno mtakuwa mnagawana mshahara na magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…