Naam hakuna tofauti yeyote kwa foleni ya dar siku hizi naona bora mtu kuendesha baiskeli kuliko kuendesha V8 katikati ya jiji la Dar.
Umezungumzia distance from Tegeta to Nyerere road maeneo haya yana foleni sana asubuhi na jioni kuanzia mwenge, morocco kwenda tangi bovu. Ushauri wangu unaweza kuendesha baiskeli in between and then kuendelea huko ukachukua gari lako ulilopaki mwenge kwenda zako nyerere road. Wakati wa kurudi kutoka kazini pia unaendesha gari yako mpaka mwenge unalipaki na kuchukua baiskeli au daladala mpaka kwako Tegeta.
Binafsi mwakani mungu akipenda nimeweka malengo nianze kuendesha baiskeli kutokea mahali nakopaki gari yangu hadi ofisini kwangu. Kwani kuanzia mjini (city centre) mpaka ofisini natumia dk 15 kutembea kwa miguu ila kwa gari it takes around 1 hour or 30 minutes. Gari yangu ni CC 2900 na hivyo inamaana kwa safari ya pole pole naweza kuwa natumia si chini ya Tshs 10,000. Bado sijaweka hasara ya gharama za kulika kwa clutch, accelerator, mikwaruzo ya gari nk. Tuseme kama 50,000. Hivyo nitalichukua gari langu hadi karibia na mjini napaki nachukua baiskeli naingia nayo katikati ya mji.
Na wewe jipange ndugu gari yeyote ina faida zake na hasara zake asikudanganye mtu. Nimeendesha gari ya CC 1100 (Suzuki Jimmy), Nimeendesha gari ya CC 2000 , Nimeendesha gari ya CC 1500 na sasa naendesha gari ya CC 2900 sioni tofauti yeyote ni nidhamu ya matumizi tu ndio cha msingi hakuna zaidi.