Gari la Mbunge ladaiwa kubeba wahamiaji haramu Mkoani Kilimanjaro

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
Wimbi la magari ya kifahari kutumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, linazidi kushika kasi nchini na safari hii gari linalodaiwa kuwa la Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likikamatwa na wahamiaji haramu saba.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilikamatwa jana saa 2:00 asubuhi katika hoteli moja iliyopo Njiapanda ya Himo, Barabara ya Moshi-Dar es Salaam Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wakati likikamatwa, mbunge huyo hakuwemo ndani ya gari.

Alipotafutwa na Mwananchi, Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Fakih Nyakunga amekiri kuwepo kwa tukio hilo na ameomba apewe muda mpaka leo Jumatano, ndiyo alizungumzie suala hilo kwa kina baada ya kukusanya taarifa kamili.

“Ni kweli kuna tukio kama hilo. Naomba tuonane kesho (leo) nikishaweka mambo vizuri. Siwezi kuzungumza hapa kwa sasa. Kuna mambo hayajakaa sawa ila kweli hilo tukio (la kukamatwa kwa gari la Mbunge) lipo,” amesema Kamanda Nyakunga.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa hazikuzaa matunda, kila alipopigiwa simu alijibu yuko kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.

Taarifa kutoka eneo la tukio, zilidokeza kuwa wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikamatwa jana asubuhi nje ya hoteli hiyo iliyopo Njiapanda na ndani ya gari walikutwa wahamiaji haramu saba.

Kulingana na taarifa hizo, hoteli hiyo inazo kamera za ulinzi (CCTV), ambapo kulingana na mienendo ya dereva wa gari hilo na taarifa ambazo polisi walikuwa nazo, walilizingira gari hilo na kuwakuta wahamiaji hao.

“Huyu dereva alikuja, akaegesha gari hapo nje akashuka kwenda kununua vocha kwa ajili ya simu yake. Hata hivyo, inaonekana polisi walikuwa wakilifuatilia kwa sababu baada ya kupaki haukupita muda, maofisa hao walijitokeza,” kimedokeza chanzo chetu kutoka eneo la tukio.

Dereva huyo aliporudi kwenye gari, baada ya muda mfupi alitokomea kusikojulikana na uchunguzi wa awali unaonyesha gari hilo linamilikiwa na mbunge (jina lake linahifadhiwa kwa sasa).

“Baada ya kubainika kuwa ni gari ya mbunge (jina tunalo) ndiyo sasa mawasiliano ya wakubwa yakafanyika, kwa hiyo hatujui nini kinaendelea ila ukiwauliza Polisi au Uhamiaji utapata nini kinaendelea,” kilidokeza chanzo hicho.

Chanzo: MWANANCHI
 
Hatuwezi kufikia uamuzi tu na kuhukumu
Lori langu niliweka tracking baadae nikaona liko sehemu tofauti kumbe anahamisha mahindi ya jamaa (dili lake)

Lakini boss na dereva kuwa marafiki sio vizuri kwa afya ya kazi zenu
Kuna wengine wanawatumia kuwa makuwadi wao mpaka wanawaachia magari weekend yote
Kuna shida sehemu
Na sipo hapa kukurupuka wala kumkandia mtu au kumtetea
 
CCM ni majambazi na ni laana kwa nchi.
Wabunge ni sehemu ndogo tu ya viongozi wanotumia nyadhifa zao kupata kinga ya biashara ovu zao.
Wapo wengi tu na wanajulikana mpaka kwenye vyombo vya dola, lakini wote ni wale wale ndio maana wanalindana.
 
Huyo mjinga hata akichelewa kuingia kwenye siku zake anaisingizia Chadema.
Kuna jamaa fulani wawili kabla ya kuingiaga kuwa wabunge wao biashara za ilikuwa magendo,washapitisha sana magendo huko mipakani na wakatengeneza sana hela
Badaye wakaingia kwenye siasa,wakawa wabunge...tena huko ccm ,sasa watu aina hiyo wakiwepo unategemea nini(ila naona sahv bungeni hawapo sijui wmetemwa)

Ova
 
Wimbi la magari ya kifahari kutumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, linazidi kushika kasi nchini na safari hii gari linalodaiwa kuwa la Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likikamatwa na wahamiaji haramu saba.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilikamatwa jana saa 2:00 asubuhi katika hoteli moja iliyopo Njiapanda ya Himo, Barabara ya Moshi-Dar es Salaam Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wakati likikamatwa, mbunge huyo hakuwemo ndani ya gari.

Alipotafutwa na Mwananchi, Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Fakih Nyakunga amekiri kuwepo kwa tukio hilo na ameomba apewe muda mpaka leo Jumatano, ndiyo alizungumzie suala hilo kwa kina baada ya kukusanya taarifa kamili.

“Ni kweli kuna tukio kama hilo. Naomba tuonane kesho (leo) nikishaweka mambo vizuri. Siwezi kuzungumza hapa kwa sasa. Kuna mambo hayajakaa sawa ila kweli hilo tukio (la kukamatwa kwa gari la Mbunge) lipo,” amesema Kamanda Nyakunga.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa hazikuzaa matunda, kila alipopigiwa simu alijibu yuko kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.

Taarifa kutoka eneo la tukio, zilidokeza kuwa wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikamatwa jana asubuhi nje ya hoteli hiyo iliyopo Njiapanda na ndani ya gari walikutwa wahamiaji haramu saba.

Kulingana na taarifa hizo, hoteli hiyo inazo kamera za ulinzi (CCTV), ambapo kulingana na mienendo ya dereva wa gari hilo na taarifa ambazo polisi walikuwa nazo, walilizingira gari hilo na kuwakuta wahamiaji hao.

“Huyu dereva alikuja, akaegesha gari hapo nje akashuka kwenda kununua vocha kwa ajili ya simu yake. Hata hivyo, inaonekana polisi walikuwa wakilifuatilia kwa sababu baada ya kupaki haukupita muda, maofisa hao walijitokeza,” kimedokeza chanzo chetu kutoka eneo la tukio.

Dereva huyo aliporudi kwenye gari, baada ya muda mfupi alitokomea kusikojulikana na uchunguzi wa awali unaonyesha gari hilo linamilikiwa na mbunge (jina lake linahifadhiwa kwa sasa).

“Baada ya kubainika kuwa ni gari ya mbunge (jina tunalo) ndiyo sasa mawasiliano ya wakubwa yakafanyika, kwa hiyo hatujui nini kinaendelea ila ukiwauliza Polisi au Uhamiaji utapata nini kinaendelea,” kilidokeza chanzo hicho.

Chanzo: MWANANCHI
Hizo ndizo sifa kuu za viongozi wa Ccm.
Yaani ndio maana wana toana roho kwa ajili ya vyeo ili walindwe kwa mauchafu yao.
 
Ukiona mwaccm hasa hawa wenye vijisent ,jua ndani ya giza wanafanya makubwa,baba mwizi mpaka wajukuu wezi
 
Hapo njiapanda ya Himo imezungukwa na wabunge wa Kilimanjarona na Tanga!!!!

Je, ni mbunge jimbo gani kati ya haya?
1. Rombo
2. Vunjo
3. Marangu
4. Mwanga
5. Same
6. Korogwe
6. Lushoto
7. Bumbuli
8.Handeni
9. Muheza
10. Moshi vijijini
11. Moshi mjini

Au ni mbunge wa mpakani na Zambia?
1. Tunduma
2. Katavi
3. Mbeya
4. Songwe
5. Ileje

Tutashangaa endapo hilo gari halitataifishwa na mmiliki kuwajibishwa kwa kosa la 'Human Trafficking'

*Tuna viongozi walafi sana, tunawalipa mishahara, posho nk lakini bado wanahujumu uchumi wa nchi kwa kufanya biashara zisizo halali
 
Huyo mbunge wa ccm ndiyo biashara zake.anajihusisha na hiyo biashara toka 2022 na Huwa anakamatwa na anaachiwa Kwa kigezo Cha kulinda heshima yake.hata Sasa hao uhamiaji lazima watakanusha tu.tumechoka kuongozwa na wahuni Kama hawa
 
Hana jina?
 
Wimbi la magari ya kifahari kutumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, linazidi kushika kasi nchini na safari hii gari linalodaiwa kuwa la Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likikamatwa na wahamiaji haramu saba.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilikamatwa jana saa 2:00 asubuhi katika hoteli moja iliyopo Njiapanda ya Himo, Barabara ya Moshi-Dar es Salaam Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wakati likikamatwa, mbunge huyo hakuwemo ndani ya gari.

Alipotafutwa na Mwananchi, Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Fakih Nyakunga amekiri kuwepo kwa tukio hilo na ameomba apewe muda mpaka leo Jumatano, ndiyo alizungumzie suala hilo kwa kina baada ya kukusanya taarifa kamili.

“Ni kweli kuna tukio kama hilo. Naomba tuonane kesho (leo) nikishaweka mambo vizuri. Siwezi kuzungumza hapa kwa sasa. Kuna mambo hayajakaa sawa ila kweli hilo tukio (la kukamatwa kwa gari la Mbunge) lipo,” amesema Kamanda Nyakunga.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa hazikuzaa matunda, kila alipopigiwa simu alijibu yuko kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.

CHANZO: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom