raraa reree
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 11,504
- 35,520
Ni kama hawa madereva wa malori anapeleka mzigo mkoani akirudi gari ipo tupu ana fanya mishe zake likikwama chimbo au mzigo wa magumashi umekamatwa ndani ya gari yeye ana kimbia msala unakuwa kwa bossMimi navyojuwa,ukisha kuwa mtu wa magumashi always utakuwa mtu wa magumashi,kuacha ni ngumu
Yaani mnataka kusema mmiliki wa gari hajuwi lolote kuhusu huyo dereva wake au labda tuseme ndy ilikuwa dili lake la kwanza
Ova
Wale madereva wengi maloriNi kama hawa madereva wa malori anapeleka mzigo mkoani akirudi gari ipo tupu ana fanya mishe zake likikwama chimbo au mzigo wa magumashi umekamatwa ndani ya gari yeye ana kimbia msala unakuwa kwa boss
Yap inaweza kuwa ndio kama huyu sasaWale madereva wengi malori
Hizo dili wao wanajiongezaga
Ova
Kwanini jina la mb wameliweka kapuni 😄Yap inaweza kuwa ndio kama huyu sasa
Umtaje wakt hausiki mwandishi hataki kesi 😄Kwanini jina la mb wameliweka kapuni 😄
Ova
Huko ndani ndani kuna watu maalum wanawapokea hao wahamiaji haramu,kuna vituo watu wanavi controlUmtaje wakt hausiki mwandishi hataki kesi 😄
Ttz wasipo thibitiwa napo wanaweza kuweka makazi hapa yakaanza kutokea mengineHuko ndani ndani kuna watu maalum wanawapokea hao wahamiaji haramu,kuna vituo watu wanavi control
Huu mtandao ni wa macartel
Na mamafia haswaaaa
Ili serikali iondokane na hali hii sijui unawakamata kuwafunga,kuwalisha huko magerezani...ni kujitia gharama tu
Watu wenyewe wao wanapita tu tz...
Wawe wanalipisha pass tu wao waendeleee
Ova
Hawa wabunge uchwara wanatuaibisha sisi wenye V8 tulizozigharimia kwa pesa ndefu!Wimbi la magari ya kifahari kutumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, linazidi kushika kasi nchini na safari hii gari linalodaiwa kuwa la Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likikamatwa na wahamiaji haramu saba.
Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilikamatwa jana saa 2:00 asubuhi katika hoteli moja iliyopo Njiapanda ya Himo, Barabara ya Moshi-Dar es Salaam Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wakati likikamatwa, mbunge huyo hakuwemo ndani ya gari.
Alipotafutwa na Mwananchi, Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Fakih Nyakunga amekiri kuwepo kwa tukio hilo na ameomba apewe muda mpaka leo Jumatano, ndiyo alizungumzie suala hilo kwa kina baada ya kukusanya taarifa kamili.
“Ni kweli kuna tukio kama hilo. Naomba tuonane kesho (leo) nikishaweka mambo vizuri. Siwezi kuzungumza hapa kwa sasa. Kuna mambo hayajakaa sawa ila kweli hilo tukio (la kukamatwa kwa gari la Mbunge) lipo,” amesema Kamanda Nyakunga.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa hazikuzaa matunda, kila alipopigiwa simu alijibu yuko kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.
Taarifa kutoka eneo la tukio, zilidokeza kuwa wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikamatwa jana asubuhi nje ya hoteli hiyo iliyopo Njiapanda na ndani ya gari walikutwa wahamiaji haramu saba.
Kulingana na taarifa hizo, hoteli hiyo inazo kamera za ulinzi (CCTV), ambapo kulingana na mienendo ya dereva wa gari hilo na taarifa ambazo polisi walikuwa nazo, walilizingira gari hilo na kuwakuta wahamiaji hao.
“Huyu dereva alikuja, akaegesha gari hapo nje akashuka kwenda kununua vocha kwa ajili ya simu yake. Hata hivyo, inaonekana polisi walikuwa wakilifuatilia kwa sababu baada ya kupaki haukupita muda, maofisa hao walijitokeza,” kimedokeza chanzo chetu kutoka eneo la tukio.
Dereva huyo aliporudi kwenye gari, baada ya muda mfupi alitokomea kusikojulikana na uchunguzi wa awali unaonyesha gari hilo linamilikiwa na mbunge (jina lake linahifadhiwa kwa sasa).
“Baada ya kubainika kuwa ni gari ya mbunge (jina tunalo) ndiyo sasa mawasiliano ya wakubwa yakafanyika, kwa hiyo hatujui nini kinaendelea ila ukiwauliza Polisi au Uhamiaji utapata nini kinaendelea,” kilidokeza chanzo hicho.
Chanzo: MWANANCHI
Wale hawana mpango kbs na tzTtz wasipo thibitiwa napo wanaweza kuweka makazi hapa yakaanza kutokea mengine
Uko sahihi pengine mbunge yeye Hana taarifa kuhusu Mambo kama hayo...anashitukizwa Tu kama AZAM Kwenye kombe la siiaraDIBII.Hatewezi kufikia uamuzi tu na kuhukumu
Lori langu niliweka tracking baadae nikaona liko sehemu tofauti kumbe anahamisha mahindi ya jamaa (dili lake)
Lakini boss na dereva kuwa marafiki sio vizuri kwa afya ya kazi zenu
Kuna wengine wanawatumia kuwa makuwadi wao mpaka wanawaachia magari weekend yote
Kuna shida sehemu
Na sipo hapa kukurupuka wala kumkandia mtu au kumtetea
HatareeCCM ni genge la wahuni
Kweli kabisa, ila watu wepesi sana kuhukumuUko sahihi pengine mbunge yeye Hana taarifa kuhusu Mambo kama hayo...anashitukizwa Tu kama AZAM Kwenye kombe la siiaraDIBII.
kumbe hayo magari yanaweza kwenda umbali mrefu bila kua na mhusika, nilijua linapoenda basi mheshimiwa hawi mbali naloUko sahihi pengine mbunge yeye Hana taarifa kuhusu Mambo kama hayo...anashitukizwa Tu kama AZAM Kwenye kombe la siiaraDIBII.
Kwani Kuna mbunge wa chadema kwa Sasa au Ni akili tu huna?Chadema ni janga
Hata akipata mimba atasingizia chadema.Huyo Etwege hata akichelewa kuingia kwenye siku zake anaisingizia Chadema.