Gari la mbunge wa Songwe lachomwa moto na watu wasiojulikana

Ndo huyu aliyetaka aongezewe posho? tena alipwe kwa dola, au ni mwingine....
 
Nchi hii siasa zishatuharibu mzee

Ova
 
Mbunge kapiga hesabu kaona kalipia bima kubwa (comprehensive) kiasi cha kununua gari nyingine. Halafu ya kwake imechoka, kaona isiwe tabu. Kalichoma, halafu mleta mada anawaangushia zigo chadema.
Sidhani kama bima ni wajinga kiasi hicho....
 
Sidhani kama bima ni wajinga kiasi hicho....
Hawana namna mkuu lazima wamlipe. Unawasha njiti ya kiberiti unatupia ndani ya gari karibu na kibanda cha kuchomea chips halafu unawaambia bima cheche ya moto wa chips ndiyo chanzo. Unavuta mkwanja
 
Hawana namna mkuu lazima wamlipe. Unawasha njiti ya kiberiti unatupia ndani ya gari karibu na kibanda cha kuchomea chips halafu unawaambia bima cheche ya moto wa chips ndiyo chanzo. Unavuta mkwanja
Sasa bima ndo watakuwa wamekuagiza kupeleka gari karibu na jiko la chipsi? itabidi ujipange sana kuwaelewesha vinginevyo hesabu maumivu.
 
Moderator Ni vyema hizi habari za kutuhumu na kuhisi bila ushahid ziwe banned manake ni kinyume na ethics za JF zilizoainishwa kwenye guidelines.
 
Tuangalie tulipojikwaa kama Taifa. CCM , CHADEMA na wenzi wao wote sio muhimu wala wakubwa kama Tanzania. Tukumbuke hivyo kila wakati na tutende accordingly. Mwenye masikio na asikie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…