Gari lililobeba mzigo upi unapenda lipate ajali karibu na nyumbani kwenu?

Alubati

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2016
Posts
6,535
Reaction score
14,840
Nakumbuka miaka ya 2000 mwanzoni lilipata ajali gari lililobeba kontena la magodoro lilipata ajali kijijini kwetu,asalalee ....kama kuna mtu analalia ngozi pale kijijini atakuwa na laana! Bahati nzuri hakufariki mtu kwenye ajali ile na pia hawakufatillia mzigo wao maana wanakijiji kila mtu alibeba godoro lake,yalikaribia 4000 hivi.

Same year likapiga chini kontena la matairi mapya ya magari,kama kawa baada ya kuhahikisha majeruhi tumewawaisha hospitali, likavunjwa kontena,tukaanza kubingilisha matairi kila mtu na njia yake, tulishanogewa na magodoro kwahiyo ajali ilishakuwa fursa.

But this time polisi hawakutuacha salama,mbaya zaidi matairi hayo tuliyahifadhi majumbani,walipiga ambush ya kibabe na msafara wa magari ya kutosha,ilikuwa mshike mshike, walibaki watoto na kinamama peke yao pale kijijini kwa muda wa wiki mbili.

Vipi mdau wewe ungependa gari lenye mzigo upi lipate ajali karibu na nyumbani kwenu? (Ila kusiwe na vifo tafadhali),

Gari linalopeleka mishahara benki? Lenye maboksi ya iphone? Au la mafuta ya petroli,unakumbuka mshike mshike wa jamaa kule mbeya lilipopata ajali tenki la mafuta likalipuka? Kudadeki moto unakukimbiza kila utapokwenda.R.I.P kwakweli.

Uzi teyari...
 

Hao wanaokunywa hivyo vinywaji kwenye chupa hawajui kama wanaweza kunywa na vipande vya chupa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…