Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
Gari lililopata kumilikiwa na watu wengi si zuri kwa matumizi, maana kila utakapopita nalo, basi ni lazima tuu utakutana na watu wanaojitapa kulijua vizuri kwa sababu walipata kulitumia.
Wapo watakaoelezea namna walivyokuwa wakiliburuza kwa mwendokasi, wengine wakijinasifu kwa mitindo mbalimbali ya uendeshaji waliokuwa wakitumia, nk.
Kwakifupi ni hivi, idadi ya wamiliki wa gari ikiwa kubwa, basi hufanya hata THAMANI yake kupungua, lakini pia hufanya uwezekano wa gari hilo kutodumu barabarani kwa muda mrefu.
Sasa basi, kwa nyie mnaojipanga kununua magari, inashauriwa kwamba ikiwa utakosa gari mpya, basi walau uchague ambalo halijamilikiwa na watumiaji wengi.
Credit 👉 maundumwingizi
✍️By Abdulatif Mohamed Kiyota