Gari limeacha njia na kuparamia fremu za maduka Ubungo Riverside

Gari limeacha njia na kuparamia fremu za maduka Ubungo Riverside

Halafu hitimisho la polisi watasema break zilifeli
Hii ndio kauli yao kwenye ajali nyingi
Gari halina break tu au matairi yameisha kabisa ila hawasemi haya je ni rushwa imetamalaki au hawana mda wa kuchunguza ajali?
Nchi masikini shida sana yaani hata wakaguzi hakuna kisa kitengo hakiwekewi hela za kutosha
 
bora imetokea asubuhi,vp kama hiyo ajali ingetokea jioni au usiku ni maafa kiasi gani yangekuwa..barabara nyingi mjini zimegeuzwa eneo la biashara mida ya jioni mm najiuliza sana kwa jinsi wanavyojipanga vile ikitokea gari kufeli breki au kuhama njia..japo kweli riziki ngumu ila kujihami kwa taadhari pia muhimu
 
sehemu za bahari ni kwamba inatakiwa uwe mita 60 hadi 90 ,inabidi pia waweke sheria za barabarani nyumba/fremu inatakiwa iwe mita 30 kutoka kwenye barabara.

Sheria ya mita kadhaa toka katikati ya barabara ipo, huenda serikali ina hofu ya kupitisha bomoa bomoa kwa "wapiga kura"...
 
sehemu za bahari ni kwamba inatakiwa uwe mita 60 hadi 90 ,inabidi pia waweke sheria za barabarani nyumba/fremu inatakiwa iwe mita 30 kutoka kwenye barabara.
Watu hawasikii hilo huku Porini kuna bikon kabisa zinasema Mwisho wa Hifadhi ya Barabara watu wamevuka bikon wanajenga mabanda yao ndani ya bikon yaan mtu inabidi atoke mita zisizopungua 30 kutoka ile bikoni ila hilo watu hawataki wanataka wakae barabarani sio mbali na barabara, na muda fulani ajari ni ajari ajari haina macho inaweza ikakukuta popote tu kikubwa umakini unahitajika
 
Watu wabishi

Ova
 
sehemu za bahari ni kwamba inatakiwa uwe mita 60 hadi 90 ,inabidi pia waweke sheria za barabarani nyumba/fremu inatakiwa iwe mita 30 kutoka kwenye barabara.
Uzembe tu wa nchi hii. Huyu amepita kijazi interchange kwa mwendo kasi likamshinda . Ilitakiwa iwe marufuku kwa malori kupita juuu ya daraja.
 
Gari lenye namba za usajili T405 DPJ limeacha njia na kuparamia fremu za maduka na mabucha ya samaki eneo la Ubungo Riverside Jijini Dar es salaam asubuhi leo December 02,2024.

Hadi sasa majeruhi wanne waliokuwa ndani ya fremu hizo wametolewa na jitihada za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Wananchi kuwaokoa Watu wengine walio ndani ya fremu zinaendelea.

hv ule ujenzi wa ring road ilikuwaje tena, si haya mavyuma yagehamishiwa yapite huko,....
 
Back
Top Bottom