Mkuu ukisema gari lako linatoa moshi! !! Ni too general, jaribu kuwa specific ni.moshi wa rangi gani, let's say kwa kesi yako na assume gari ni la petroli !!!!
Iko hivi;
1: moshi. Ni mweusi. ... hapa una tatizo la fuel na system zake, kufix ni cheap but time consuming na inaitaji fundi mzuri
2: moshi ni mweupe. ... hayo mambo ya ring piston na compression hapa sasa ndo unabidi ujipange kwa engine overhaul, labda kama una bahati unaweza kuta ni valve seals tu zimechoka ndio unaweza kupata nafuu otherwise ni maumivu ya hela...
3: moshi wa blue. . Hapo utakuwa na matatizo yote mawili kwa mpigo, ni pasua kichwa sana hii scenario kuliko hizo mbili zilizotangulia, hapa kama una hela mchagoni nashauri tafuta used engine pachika , lasivyo itakugharimu sana.
NB. Kama gari lako ni la diesel, namba moja na mbili ni kawaida sana kwa magari hayo kutegemeana na hali ya hewa, hasa majira ya baridi, lakini kwa moshi aina ya tatu, bado ni majanga.