Gari Nissan Dualis/ Qashqai kuchelewa kuchanganya

Anaongea kama Toyota haziendi garage.
Mimi nimetumia dualis miaka mitatu haijawah kuniletea shida hadi nikauiza na niliyemuuzia haijamsumbua katumia miaka miwili na ameshaiuza na yeye tena kaiuza kwa sababu kapata shida ya hela ila hakuuza kwa kupenda
 
Wewe umeongea kimihemko zaidi na siyo kiufundi....

Suala la gari kuungua kuna mambo mengi..

Gari limetoka Japan, linafika bongo watu wanafanya modifications za wiring, sijui wanafunga mataa taa, music kihuni, sijui alarm za kichina, gari likiwaka moto utalaumu..?

Suala lingine, Nissan hazitaki ukanjanja...hazitaki spea za kufananishia au kupimishia...
Kwa mfano Nissan hazitaki zile spark plugs za elfu 4 ambazo unaweza kufunga kwenye Toyota, hata engine oil kuna baadhi ya Nissan zainachagua, gear box ndiyo usiseme.....hapa ndiyo wabongo hawapendi...

Sasa kama Nissan tu mnalalamika, gari za ulaya mtaziweza..?

Haya hii hapa iliyoungua nayo ni Nissan..?
Gari lolote linaweza kuhngua mahala popote

Nissan ni gari nzuri sana ukifuata kanuni za kulitunza.
 
Kwa uhakika zaidi, tafuta fundi mzuri fanya diagnosis..

Ukikuta hamna fault yoyote, basi badilia airfilter, spark plugs funga kama zilizokuja na gari..
Injini kama umeweka oil ya SAE40, kabadili haraka uweke 5w30 au 5w40 ufurahie maisha..
 
Kwa uhakika zaidi, tafuta fundi mzuri fanya diagnosis..

Ukikuta hamna fault yoyote, basi badilia airfilter, spark plugs funga kama zilizokuja na gari..
Injini kama umeweka oil ya SAE40, kabadili haraka uweke 5w30 au 5w40 ufurahie maisha..
Okay mkuu....

Ila engine ina 5w30...

Nitafanya diagnosis.
 
Mkuu uliongea kweli Duuuh kweli majanga
 
Hamna gari humo.. hizo nissan zote ni takataka tu , juzi dualis limeungua huko watu wana hahana inaelekea hata kuliuza itakuja kuwa ishu sana
 
Mkuu uliongea kweli Duuuh kweli majanga
Sijawahi kukurupuka nimetumia hizo gari hivyo naelewa , nadhani mmeona last week millardAyo kuna na nyingine imewaka huko mbezi beach tangi bovu mchana kweupeeee, kuna mdada naye mbishiiiii juzi kati yakwake imewaka ikiwa parking uani tena haijawashwa. watu waache ubishi na ujuaji kwa hali ilivyo ngumu sasa mtu aunguliwe na gari stress zake si zinapunguza miaka kadhaa ya kuishi? Pole zao wabishi.
 
Umetumia mwaka gani? Zako ziliwaka ngapi?
 
Hapana. Gear box oil haijabadilishwa. Gari ina miezi miwili hapa bongo.

Haijawahi kuguswa popote zaidi ya kumwaga oil tu ya engine.
Hata huko nje kuwa wamiliki wa magari wasiojua kutunza magari wanayaharibu kama huku tu.
 
Why not spark plug zinakua zimeanza kuchoka?
Hapana ni mfumo wake inatakiwa ukiamshie taratibu. Hata gari za kawaida pia haishauriwi uivurumue kama unakimbizwa na polisi.

Anza kwa kuichochea taratibu hadi ikashika speed then inaendelea kushika speed.
 
Sasa wewe una ajenda yako binafsi. Magari hayo unayaongelea kama yana default wakati ni changamoto za maintenance na uzembe wa wamiliki.
 
Naomba uedit hapo "hakuna ngoma wala sufuria" isomeke "hakuna ngoma wala tarumbeta" [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Okay so solution ni nini?
Hapo baada ya kuchanganya ni sahii huwa ipo kibati sana..
Huyu rafiki yako atakuwa ndio wale akiingia kwenye gari anakishaweka D anataka avurumue gari itoke huku tairi zinaslip kwenye ardhi au itoke na makelele ya tairi inapiga ukelele kwenye lami.

Jambo ambalo si zuri.
 
Bora umemuumbua maana kaja hapa na story za vijiweni. Huyu atakuwa ni wale mafundi magari wa chini ya muembe hizi gari huwa zinawashinda kutengeneza so huwa wanaziponda maana wateja wakizinunua wao wanakosa biashara.
 
Kwa uhakika zaidi, tafuta fundi mzuri fanya diagnosis..

Ukikuta hamna fault yoyote, basi badilia airfilter, spark plugs funga kama zilizokuja na gari..
Injini kama umeweka oil ya SAE40, kabadili haraka uweke 5w30 au 5w40 ufurahie maisha..
Hii gari ina Engine oil yake specific na Gear box oil yake specific.
 
Hamna gari humo.. hizo nissan zote ni takataka tu , juzi dualis limeungua huko watu wana hahana inaelekea hata kuliuza itakuja kuwa ishu sana
Kila mtu analitolea story gari moja kuungua. Kwani ndio gari la kwanza kuungua. Mimi nimeshakutana na gari kibao za Toyota zinaungua humo mabarabarani. Ila haiwezi kuwa sababu ya hizo gari hazifai.
 
Mmmh CVT transmission inachelewa kuchanganya ?
Ukiifurumusha haipokei moto haraka hivyo maana ile haina mfumo wa gear (counter gear) ile inatumia mfumo wa pulleys na chain so inabalance nguvu ya gari na mzigo. Ukiwa unaendesha inabalance nguvu ya gari na wepesi wa body kadiria kasi ikiongezeka.

Ndio maana mafuta hizi gari hazichomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…