Gari Nissan Dualis/ Qashqai kuchelewa kuchanganya

Gari Nissan Dualis/ Qashqai kuchelewa kuchanganya

Sijawahi kukurupuka nimetumia hizo gari hivyo naelewa , nadhani mmeona last week millardAyo kuna na nyingine imewaka huko mbezi beach tangi bovu mchana kweupeeee, kuna mdada naye mbishiiiii juzi kati yakwake imewaka ikiwa parking uani tena haijawashwa. watu waache ubishi na ujuaji kwa hali ilivyo ngumu sasa mtu aunguliwe na gari stress zake si zinapunguza miaka kadhaa ya kuishi? Pole zao wabishi.
Wewe unaonekana hizi story zako unaokoteza sana. Hiyo gari iliyorushwa kwenye habari na milard ayo kila mtu anasema hiyo hiyo.

Unless una takwimu ya hizi gari kuungua kila wiki au kila siku usiongee kwa kujiaminisha kuwa hizi gari zina factory error ya kuzifanya ziungue bila sababu.
 
Nasema ivi NISSAN ni kichefuchefu kwa Africa, taka usitake. Ikianza kuzingua, safari za garage haziishi na mfuko uwe njema muda wote.
 
Wewe unaonekana hizi story zako unaokoteza sana. Hiyo gari iliyorushwa kwenye habari na milard ayo kila mtu anasema hiyo hiyo.

Unless una takwimu ya hizi gari kuungua kila wiki au kila siku usiongee kwa kujiaminisha kuwa hizi gari zina factory error ya kuzifanya ziungue bila sababu.
naongelea experirnce mimi mwenyewe yangu imewaka sasa wewe ambaye huna hata baiskeli unadandia tu nyuzi ili uonekane upo kalagabaho
 
naongelea experirnce mimi mwenyewe yangu imewaka sasa wewe ambaye huna hata baiskeli unadandia tu nyuzi ili uonekane upo kalagabaho
Huwezi kukosa picha. Hebu tuonyeshe hapa tujiridhishe. Halafu usiwe unachukulia watu kawaida sana, unaweza kukosa au kupitwa na vitu vizuri sababu ya kuchukulia watu poa. Unaonekana kwako Gari ni anasa.
 
Dualis katika ubora wake,ila kifupi hizi gari hazijawahi kunivutia,hasa dashboard yake,ingawa kibongo bongo zina trend kwelikweli....
 
Wewe umeongea kimihemko zaidi na siyo kiufundi....

Suala la gari kuungua kuna mambo mengi..

Gari limetoka Japan, linafika bongo watu wanafanya modifications za wiring, sijui wanafunga mataa taa, music kihuni, sijui alarm za kichina, gari likiwaka moto utalaumu..?

Suala lingine, Nissan hazitaki ukanjanja...hazitaki spea za kufananishia au kupimishia...
Kwa mfano Nissan hazitaki zile spark plugs za elfu 4 ambazo unaweza kufunga kwenye Toyota, hata engine oil kuna baadhi ya Nissan zainachagua, gear box ndiyo usiseme.....hapa ndiyo wabongo hawapendi...

Sasa kama Nissan tu mnalalamika, gari za ulaya mtaziweza..?

Haya hii hapa iliyoungua nayo ni Nissan..?
Gari lolote linaweza kuhngua mahala popote

Nissan ni gari nzuri sana ukifuata kanuni za kulitunza.View attachment 2172349
Hii ilikuaje mkuu?
 
kuchelewa kuchanganya kuna sababishwa na vitu vingi. Japo mimi nilikutana nayo hyo changamoto,kupanda vilima vya Goba unakua kama unaibembeleza gari,nikahangaika sana baadaye kuna fundi yupo kinondoni akaniambia ishu ni Catalytic convertor imejaa uchafu mwingi sana. Waliisafisha,baada ya hapo ikawa nyepesi sana.
 
Dunia sasa hivi ni kijiji jamani
Hizi Duals hapa bongo hazizidi asilima 1 ya Duals zote duniani

Sasa zinaungua za bongo tu?
Nendeni kwenye platform reliable mkaangalie reviews zake kutoka kwa watumiaji

Shida ni kwamba una Nissan lakini unataka kui treat kama ni toyota vile
Mafundi wa kibongo nao wanalazimisha spea fake na oil fake za toyota
Wauza spea nao walewale tu na wanauza bei jui ili mradi tu

Tatizo sio gari
Tatizo na mazoea ya kitoyota
Kuepuka haya tununue tu toyota
 
Back
Top Bottom