Gari wanazohitaji waTanzania hazipatikani dunia nzima

Mkuu naona umekomaa sana.....naona huamini sijui kama naweza kumiliki bmw 320i? au
Kwenye account yangu kwenye banner picha ipo.
Utaona simu yangu ina page ya jf...........Thanks.......
320i

Inaonekana umeumia sana kusikia crown zipo kwenye kundi la ist πŸ˜… πŸ˜… πŸ˜… , ngoja tuzitoe mkuu.
 
Hahahaha hivi mi najiuliza haiwezekani kuunda gari lenye engine mbili za pikipiki hata ile ya boxer ili kuwaokoa wabongo πŸ˜‚ na adha ya kwenda sheli! Ina maana liwe na gearbox automatic gear 5 but yenye reverse gear tu lakini.
Mkuu cheap is cost, pikipiki Kama Honda CBR400 ina piston 4 inaizidi hata Passo. Sasa gari ya piston 2 ni shida.

Kuna project YouTube niliona wamechukua Isuzu KB single cabin wameiwekea injini ya power tiller ya single piston ya kuwasha kwa hendeli.

Ukiwa unaendesha hiyo mitikisiko mbavu, meno na pumbu zitakavyochezeshwa ukishuka mwili unatetemeka Kama Nokia au Philips.
 
Maana ndugu zangu wanapenda sana kitonga cha sheli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!!!
Kuhusu mtetemo ni kufunga mounting zenye mpira laini tu.
 
Mjapan ana mawe ya hatari sana, sina mashaka kabisa na uwezo wa mjapan. Corolla zipo njema sanaaa. Ila wajeruma watasema ni taka taka
Mkuu Toyota Corolla ndiyo gari inayoshikilia rekodi kwa mauzo makubwa duniani mpaka Sasa, ikifatiwa na VW Beetle almaarufu mgongo wa chura au kobe.

Toyota Corolla imechuka tuzo nchini ujerumani miaka ya nyuma kuwa ndio gari iliyokuwa na rate ndogo ya breakdown ikilinganishwa na VW Golf.
 
SA yote hakuna fuga? Unaweza kunisaidia Kwanini hakuna fuga?
Nissan wanatengeneza FUGA kwa ajili ya soko la Japan na baadhi ya nchi za Asia tu,hapa SA salon pekee toka Nissan ni Almera. Jaribu KIA wana salons cars kali sana kama Cerato, Optima nk. Pia Hyundai Elantra ni salon nzuri tu.
 
Ahsante kwa uchambuzi, mimi binafsi huwa nina tabia ya kuuliza uliza vitu hata kama sina uwezo navyo, ndio maana nina kaujuzi kidogo kwa mbali. Nilinunua Toyota Premio ya mwaka 2000, kwa kuwa ndio uwezo wangu ulipofikia kwa sasa, lakini nina hakikisha matengenezo yake yanakuwa ya uhakika na oil ninazoweka ni za daraja la kwanza.

Nafanya hivyo kwa kuwa lengo la kununua hako kagari ni kunisaidia mimi na majirani zangu (hasa kama kuna dharula) mafuta huwa sipendi yawe chini ya nusu tank (naongeza) yaani kama sina fedha ya mafuta ni bora nitembee kwa mguu kuliko kwenda kuweka 2Ltrs (maana najua nitaifanya engine kuwa na maisha mafupi na kunigharimu zaidi baadae)
 
Nakupata Mkuu, Well Said.....
 
Wazee wa engine lita nne goma hilo
nimelikuta FB huko [emoji28]

Sema Hii crown ukisafiri nayo dar to mwanza unaenjoy sana aisee very smooth[emoji1487]
 
Wazee wa engine lita nne goma hilo
nimelikuta FB huko [emoji28]

Sema Hii crown ukisafiri nayo dar to mwanza unaenjoy sana aisee very smooth[emoji1487] View attachment 1708391
Atashusha tu hiyo bei hadi akome.. ameishalitumia alafu anauza kama lipo japan. Alafu hizo figure zipo sahihi kweli mbona hela ndefu sana hiyo ya kununua kabisa Mjepu wa kuchukulia majani shambani
 
Kumiliki gari ya zaidi ya 2500cc kwa bongo hapa ni kichefu chefu hasa kama utafikia mahala unataka kuliuza.

Hata liwe namba DVZ hamna mtu anataka gari lenye mashine kubwa namna hio labda uwauzie watoto wa kiarabu ndo wanawakaga nayo[emoji23]
Tatizo kipato Mkuu, wengi bongo vipato vya shida ila gari la cc 2500/: ni gari powerful kwa masafa sema wengi bongo ni wa zee wa ist,Porte n.k gari za cc 1300 ndo nyingi bongo hzo hzo mtu ataka kupiga nazo masafa,.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…