Gari ya Dangote yaacha njia na kuparamia nyumba, imesababisha foleni sana

Gari ya Dangote yaacha njia na kuparamia nyumba, imesababisha foleni sana

Yaani ndo nafika Nyumbani ukweli njia yetu ya Mbagala ikitokea ishu hata ndogo basi inaleta foleni.
 
Ndio kukimbilia kupost ama! si ungekusanya taarifa muhimu kisha utupe kitu kinachojitosheleza.
 
Wala tatizo sio magari ni madereva, kuna siku nimepanda nilikuwa nasafirisha mzigo tani 32,kutoka mpanda kwenda kahama tulitumia masaa 12!!!siku hiyo sitakuja isahau maishani!!! Nilitamani niteremkie njiani!! Wakawa wanasema lazima waendeshe hivyo kwani hiyo route haiko ki ofisi, ni ya kwao!!!
Ina maana magari yake hayana tracking devices mpaka madere wanafanya hayo?
 
Hii kampuni inapaswa kusimamia usail wa madereva wengi wapo pale kwa rushwa
 
Madereva wa hii kampuni wanasafiri miendo mirefu sana bila kua na Tingo wala Madereva wasaidizi. Dereva anakanyaga gia mtwara mpaka Kyaka na sio tripu moja tu
 
Ina maana magari yake hayana tracking devices mpaka madere wanafanya hayo?
Hakuna gari la dangote ambalo halina tracking device, bali wanachofanya madereva ni kutoa taarifa kuwa gari limeharibika kwenye mfumo wa betri, nyaya zimeungua hivyo amepaki polini, inabidi asubilie spea, atumiwe, hivyo anachofanya ni kuchezea hicho kifaa kwani kitakuwa hakisomi yupo wapi, anafanya yake, japo kuna baadhi ya mabosi anakula nao, kwani utaratibu waliowekewa kuna watu wamepewa kazi kuwa ukiliona tu gari la dangote labda lina mzigo ambao sio cement, piga picha warushie wahusika!!
 
Imeanguka kwa bahati mbaya tu au Hasira za Dereva labda kutokupewa Posho yake au kulipwa Mshahara kwa wakati ndiko kumesababisha hili?

Madereva wa bongo wengi ni wapumbavu, hawana uchungu wala huruma kwa mabosi wao all the time wanawaza kuiba tu. Dreva anapata posho nzuri and still haridhiki na hapo hapo anamuibia tajiri yake, isitoshe sio mtunzaji gari analipeleka na kuligongesha likiharibika tajiri yake anajua atalitengeneza 😀. Mkuu asikuambie mtu kazi ya magari ni ngumu sanaa,tena kwa hawa madreva wetu wa kibongo bongo mhhh!
 
Haya malori ya kichina Kule china yanauzwa kwa mafungu. Dangote alinunua malori 500 sawa na scania mpya 10. Akafika Tz akaitwa mwekezaji mkubwa.

Gari za mchina ni nzuri pia zinataka utunzaji tu, service kwa wakati. Scania ni rahisi sana kunoki injini endapo oil itakuwa imepungua kwa wingi, tofauti na gari za mchina mapafu ya mbwa, ni magari magumu na yana nguvu sanaa, kwenye milima inapanda kama haina akili tena kwa gia kubwa sio mchezo babaa 😀

FAW NA HOWO weka mbali na watoto.
 
Back
Top Bottom