Gari ya Tsh. 12M

Sio mtaalam sana ila kwa ushauri wangu zingatia haya
1.Upatikanaji wa spare
2.Gharama za spare
3.Fuel consumption budget yako
4.Mizunguko yako yenye kuhitaji hilo gari
5.Engine size
6.Gari inayouzika kwa haraka utakapohitaji kubadilisha au kutumia gari kutatua matatizo

Anza na IST old model, Vitz old model late version ile yenye taa za kijicho, Spacio, Toyota Allex au Runx ingawa hizo 2 za mwisho sijui bei zake.
 
Alex au Run X anunue ambazo zimesajiliwa recently kwa bei hio anapata.

DY akitafta kwa pesa yake anaipata tu ambayo imenyooka bila maumivu ya kodi za ajabu TRA ni kubadili kadi tu maisha yaende
 
Sijui gari ila spacio toleo jipya ni nzuri na imekaa vizuri. Nazungumzia udhoefu wa spacio old model sura ya baba.

Au ractic toleo jipya
 
You have said it all mzee

Nyongeza, anaweza kufikiria pia kuhusiana na carina.
 
Ushauri mzuri Sana na Uzi ufungwe

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Tofauti na IST ningekushauri kuchukua Spacio new model, around 13-14m unavuta mkoko kutoka Japan.

Usione hizo gari zimejaa barabarani huku mitaani, zina sababu zake za msingi.
Hizo spacio new model ni version ya kuanzia mwaka Gani kiongozi?
 
Yote kwa yote sikushauri kununua gari yoyote kutoka mkononi mwa mtu, unaweza kupigwa kwa kuuziwa kimeo na kikakutesa. Jipange kuvuna chuma kutoka Japan.
Mkuu hapo [emoji375][emoji375][emoji375][emoji375]
 
Ahsante mkuu Kwa ushauri,
Mkuu hivi hio IST old model au Passo inaweza kutembea dar to mwanza non stop au kupumzika tu Kwa muda mfupi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…